China yatoa mwongozo wa kuanzisha soko la ndani lenye muunganiko

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 11, 2022

BEIJING - China imetoa mwongozo wa kuharakisha uanzishaji wa soko la ndani lenye muunganiko ambalo litakuwa na ufanisi wa hali ya juu, linalofuata kanuni, ushindani wa haki, na lililo wazi.

China inalenga kukuza mzunguko na upanuzi mzuri wa soko la ndani, kukuza mazingira thabiti, ya haki, yenye uwazi na yanayoweza kufanyiwa makadirio, na kupunguza gharama za miamala ya soko.

Mwongozo huo uliotolewa kwa pamoja na Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Baraza la Serikali ya China pia unaeleza kuwa China inalenga zaidi kukuza uvumbuzi wa kisayansi na uboreshaji wa viwanda na kukuza faida mpya za kushiriki katika ushindani na ushirikiano wa kimataifa.

Juhudi zitafanywa ili kuboresha mifumo iliyounganishwa ya ulinzi wa haki za mali, ufikiaji wa soko na mfumo wa udhibiti wa jamii.

Mwongozo huo unasisitiza kukuza muunganisho wa wadau wa soko, ikiwa ni pamoja na kujenga mtandao wa kisasa wa mzunguko, kuboresha njia za kupashana habari za soko, na kuboresha majukwaa ya miamala.

China itafanya kazi kukuza soko la ndani lililounganishwa la vipengele vya rasilimali za uzalishaji, ikiwa ni pamoja na ardhi, kazi, mtaji, teknolojia, data, nishati na mazingira.

Mwongozo huo unasisitiza kuweka kanuni za pamoja za udhibiti wa soko, na kuboresha kwa kina uwezo wa usimamizi wa soko. Mwongozo unatoa wito wa kuongeza juhudi za kupambana na ukiritimba na kudhibiti mazoea ya ushindani usiyo wa haki. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha