Waziri Mkuu wa China atoa wito wa utulivu wa ajira na bei ili kukuza uchumi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 12, 2022

Waziri Mkuu wa China Li Keqiang, akiongoza kongamano kuhusu hali ya uchumi katika Mkoa wa Jiangxi, Mashariki mwa China, Aprili 11, 2022. Maofisa wa serikali kutoka mikoa ya Jiangxi, Liaoning, Zhejiang, Guangdong na Sichuan wamehudhuria kongamano hilo kupitia mtandaoni au nje ya mtandao. (Xinhua/Ding Lin)

NANCHANG - Waziri Mkuu wa China Li Keqiang siku ya Jumatatu wiki hii ametoa wito wa kudumisha utulivu wa viwango vya ajira na bei za vitu ili uchumi wa nchi uendelee kwenye kiwango kinachofaa.

Li, ambaye pia ni Mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), ameyasema hayo alipokuwa akiongoza kongamano kuhusu hali ya uchumi katika Mkoa wa Jiangxi, Mashariki mwa China, ambao maofisa wa serikali kutoka mikoa ya Jiangxi, Liaoning, Zhejiang, Guangdong na Sichuan wamehudhuria kupitia mtandaoni au nje ya mtandao.

Huku akiangazia uthabiti mkubwa wa uchumi wa China, Li amewataka watu kuendelea kufuatilia kwa karibu wakati wa mabadiliko yasiyotarajiwa na shinikizo la kushuka kwa uchumi ndani na nje ya nchi, na kukabiliana na changamoto mpya.

Li amesisitiza kwamba, sera za usaidizi kama vile marejesho na kupunguzwa kwa kodi, msaada wa kifedha kwa uchumi halisi, utoaji wa dhamana maalum za serikali, na ujenzi wa miradi muhimu unapaswa kuharakishwa ili kusaidia wadau wa soko kukabiliana na matatizo.

Amehimiza juhudi madhubuti za kukuza kilimo wakati wa majira ya mchipuko, kujitahidi kupata mavuno mengi ya nafaka kwa mwaka mzima, ili kuimarisha msingi wa bei za vitu .

“Jitihada zinapaswa kufanywa ili kuhakikisha utoaji tulivu wa umeme, makaa ya mawe na nishati zingine, na kudumisha utendakazi mzuri wa mitandao muhimu ya usafirishaji na bandari ili kudumisha uthabiti wa minyororo ya viwanda na usambazaji bidhaa” Li amesema.

Amesema kuwa hatua zinazolengwa za usaidizi zinapaswa kuwekwa wazi kwa sekta na makampuni yanayokabiliwa na matatizo -- hasa kampuni ndogo na za ukubwa wa kati, na biashara zinazomilikiwa na mtu mmoja mmoja.

Li pia amesisitiza umuhimu wa kuhakikisha ugavi wa mahitaji ya kila siku kwa watu walioathiriwa na janga la virusi vya korona, na haja ya kufanya juhudi za kukidhi mahitaji ya matibabu ya watu.

Waziri Mkuu wa China Li Keqiang, akiongoza kongamano kuhusu hali ya uchumi katika Mkoa wa Jiangxi, Mashariki mwa China, Aprili 11, 2022. (Xinhua/Ding Lin)

Waziri Mkuu wa China Li Keqiang, akiongoza kongamano kuhusu hali ya uchumi katika Mkoa wa Jiangxi, Mashariki mwa China, Aprili 11, 2022. (Xinhua/Ding Lin)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha