Umwamba wa Marekani: Mchochezi wa Msukosuko wa Dunia anayejificha

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 12, 2022

Mchoraji wa katuni: Ma Hongliang

Tangu mgongano kati ya Russia na Ukraine ulipolipuka, Marekani inaipelekea Ukraine silaha bila kusita na kuweka vikwazo dhdi ya Russia, ikichochea msukosuko mara kwa mara.

Kama ni kweli Marekani inawafuatilia watu wa Ukraine, ingefanya juhudi za kuhimiza amani, badala ya kutoa silaha tena na tena. Kitendo cha Marekani cha kuchochea msukosuko kinaficha kusudi lake baya la kuimarisha hadhi yake ya umwamba kwa kupitia kuchochea migongano.

Tukikumbuka historia tutaona kuwa, Marekani imezoea kupata faida kutoka kwenye vurugu za vita ilizozusha. Tangu nchi hiyo ilipotangaza uhuru wake Julai 4, 1776, katika historia yake ya zaidi ya miaka 240 iliyofuata, muda wake wa kutoshiriki katika vita vyovyote kwa jumla haufikii miaka 20. Kwa mujibu wa takwimu zisizokamilika, kutoka kukomeshwa kwa Vita Vikuu vya Pili vya dunia mwaka 1945 hadi mwaka 2001, migogoro ya kijeshi 248 ilitokea katika sehemu 153 duniani, na migogoro 201 kati ya hiyo ilizushwa na Marekani, ambayo ilichukua asilimia 81.

Baada ya Vita Vikuu vya Pili vya dunia, Marekani na NATO zimezusha misukosuko kote duniani kwa njia ya kuvamia na ya kuingilia: kutoka Guatemala, Cuba, Vietnam, Congo, mpaka Nicaragua, Iraq, Yugoslavia, na tena mpaka Afghanistan, Libya, Syria......kivuli cha Marekani kilionekana kila mara katika migogoro mikubwa au midogo ya kidunia, Marekani kweli ni mchochezi wa misukosuko ya dunia aliyeko nyuma ya pazia. Marekani hajali amani na maendeleo ya dunia , inazusha mara kwa mara misukosuko ni mchezo wake wa kisiasa tu kwa ajili ya kujipatia manufaa yake binafsi. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha