Umwamba wa Marekani: Inanufaika sana na vita duniani kote

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 13, 2022

(Mchoraji wa katuni: Ma Hongliang)

Tangu mgogoro kati ya Russia na Ukraine uzuke, Marekani inaendelea kuongeza mafuta kwenye moto kwa kupeleka silaha mfululizo kwa Ukraine. Katika msukosuko wa Ukraine, Marekani na viwanda vyake vya zana za kijeshi wanachuma pesa nyingi kwa kunufaika na “vita” na kuwa “washindi wakubwa.”

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Taasisi ya Utafiti wa Amani ya Kimataifa ya Stockholm ya Sweden, Marekani ambayo ni muuzaji mkubwa zaidi wa silaha ndiyo inayonufaika zaidi kutokana na mgogoro kati ya Russia na Ukraine. Bei ya hisa za mashirika makubwa ya biashara ya silaha ya Marekani inathibitisha habari hii. Kuanzia Februari 24 hadi Machi 28, Hisa za kampuni ya Lockheed Martin zilipanda kwa zaidi ya 13%, za kampuni ya Northrop Grumman zilipanda kwa zaidi ya 13.4%, na za kampuni ya General Dynamics zilipanda kwa zaidi ya 10%.

Marekani inachochea mvutano huu bila kusita na kuwa na hofu ya mgogoro huo kwisha. Lengo lake ni kuchuma pesa kutokana na vita ili kujitajirisha na kudumisha hadhi yake ya umwamba kwa muda mrefu. “Tangu mgogoro kati ya Russia na Ukraine utokee, wizara ya Ulinzi ya Marekani, Mtaa wa K (mahali ambapo makampuni yenye maslahi na ushawishi ya Washington hukusanyika), makampuni ya biashara ya silaha na ofisi za bunge la Marekani, walikuwa wakifurahia kimya kimya. ” Alisema Franklin Spinney, mchambuzi wa zamani wa mambo ya kijeshi wa wizara ya Ulinzi ya Marekani.

Marekani inachochea vita bila kusita: Vita vya Ghuba, Vita vya Kosovo, Vita vya Afghanistan na Vita vya Iraq...... watu wote waliathiriwa na kupata hasara kutokana na vita hivyo, lakini ni makampuni ya biashara za zana za kijeshi ya Marekani yanayowadhibti wanasiasa wa Marekani ndio walioshinda——walitumia hali ngumu ya maisha ya watu wa nchi nyingine kuchuma pesa nyingi. Marekani kweli ni "mnyonya damu" ambaye inapata pesa nyingi kutoka sehemu mbalimbali duniani kwa kutumia fursa ya vita na migogoro.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha