Takwimu za ushuru zaonyesha kuwa Michezo ya Olimpiki imechochea shauku juu ya michezo ya majira ya baridi nchini China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 13, 2022

BEIJING, - Michezo ya Olimpiki na Michezo ya Paralimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing 2022 imechochea shauku za watu kwa michezo ya majira ya baridi nchini China, na kusababisha kuongezeka kwa kasi kwa mapato ya mauzo ya bidhaa zinazohusiana na michezo hiyo, takwimu kutoka kwa idara ya ushuru nchini humo zinaonyesha.

Kwa mujibu wa takwimu za mapato yatokanayo na ushuru zilizotolewa na Idara ya Ushuru ya Baraza la Serikali ya China, Mwezi Machi, mapato yatokanayo na mauzo ya sekta ya michezo katika eneo la Chongli katika Mji wa Zhangjiakou, Mkoa wa Hebei na eneo la Yanqing la Beijing, ambayo yalikuwa wenyeji wa michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya 2022, yaliongezeka kwa asilimia 65 na asilimia 62.6 ikilinganishwa na Mwaka uliopita. .

Takwimu hizo zinaonesha kuwa, katika robo ya kwanza, mapato ya jumla ya mauzo ya tasnia ya michezo katika maeneo hayo mawili yalikua kwa kasi ya kwa asilimia 35.2 na asilimia 68.9 kuliko Mwaka uliopita.

Shauku ya michezo ya majira ya baridi pia ilikuza shughuli za malazi na chakula za maeneo husika na kuchochea manunuzi ya bidhaa zinazohusiana na michezo.

Sekta za malazi na chakula katika Chongli na Yanqing zimeshuhudia mapato yao yatokanayo na mauzo katika miezi mitatu ya kwanza yakipanda kwa asilimia 350 na asilimia 55.9 kutoka kipindi kama hicho mwaka mmoja uliopita. Mapato ya mauzo yatokanayo na bidhaa na vifaa vya michezo katika maeneo hayo mawili yaliongezeka kwa asilimia 61.6 na asilimia 47.3 ikilinganishwa na wakati kama huo Mwaka uliopita.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha