Marekani inakula njama kuanzisha Vita Baridi vya karne ya 21

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 14, 2022

(Mchoraji wa katuni: Ma Hongliang)

Uamuzi wa kiholela wa Jumuiya ya NATO inayoongozwa na Marekani kuhamisha kile kinachoitwa safu ya ulinzi kwa ajili ya usalama wa pamoja hadi kwenye mipaka ya Russia na Ukraine umesababisha mgogoro wa Ukraine. Hii inafichua zaidi kiini cha umwamba wa Marekani na athari za uharibifu za mawazo ya Vita Baridi ya Marekani.

Kulinda amani na utulivu wa Dunia na kikanda haijawahi kuwa kipaumbele katika mkakati wa Washington. Kuanzia katika kuimarisha uhusiano kati ya nchi za Muungano wa Macho Matano, hadi kupigia debe Mazungumzo ya Usalama ya Ushirikiano wa Pande Nne (Quad) inayojumuisha Marekani, Japan, India na Australia, Washington imeendelea kuimba kaulimbiu kuhusu ushirikiano wa pande nyingi katika kauli zake za hadharani, lakini kwa hakika imekuza "siasa za makundi" ambazo zinahuisha ukaribu na kutengwa katika miaka ya hivi karibuni.

Marekani imeanzisha ujanja wake wa siasa za kijiografia kwa kisingizio cha kukuza ushirikiano wa kikanda. Kwa kujitahidi kujenga kambi za kipekee, Washington inataka kufufua mawazo ya Vita Baridi ya nchi hiyo, ikifichua haswa nia ya kweli ya Ikulu ya Marekani ya kudhibiti maendeleo ya nchi zingine na kuimarisha nafasi yake ya umwamba katika mazingira ya kimataifa.

Licha ya kuwa miongo kadhaa sasa imepita tangu kumalizika kwa Vita Baridi, baadhi ya wanasiasa wa Marekani hawajawahi kuacha mawazo yao ya Vita Baridi. Hatua za Washington kudumisha umwamba wake wa kimataifa zimezua migawanyiko na migogoro duniani kote. Marekani, ambayo sasa ni mla njama wa Vita Baridi katika karne ya 21, ni tishio la kweli kwa amani na utulivu wa Dunia.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha