

Lugha Nyingine
Uwezo wa China wa kupima virusi vya Korona wafikia sampuli milioni 51.65 kwa siku
Wahudumu wa afya wakifanya kazi katika maabara ya kupima virusi vya Korona huko Shanghai, China Aprili 15, 2022. (Xinhua/Zhang Jiansong)
BEIJING - Mashirika ya China ya kupima virusi vya Korona sasa yanaweza kuchakata sampuli milioni 51.65 kwa siku, Kikundi kazi cha pamoja cha mfumo wa kudhibiti na kukinga UVIKO-19 cha Baraza la Serikali la China kimesema jana Jumapili.
Upimaji wa virusi vya Korona wa umma kwa wingi umekuwa nyenzo madhubuti ya kugundua maambukizi ya UVIKO-19 nchini China na uwezo mkubwa utaongeza imani ya watu kudhibiti janga hilo, kikundi kazi hicho kimesema katika taarifa yake kwa vyombo vya habari.
“Hivi sasa nchini China kuna mashirika 13,100 yaliyoidhinishwa kupima virusi vya Korona, na karibu watu 150,000 wanafanya kazi hii ya upimaji” inasema taarifa hiyo.
Kwa ujumla, majibu ya vipimo yanaweza kutolewa ndani ya saa sita, na idara za afya zimeendelea kufanyia kazi mikakati ya kupima haraka.
Kikundi kazi hicho kimesema, mashirika ya kupima virusi vya Korona yanafanya kazi na uwezo wao wa juu zaidi kukabiliana na mlipuko wa hivi punde zaidi huko Shanghai. Mji huo umefanya raundi kadhaa za upimaji wa umma tangu mapema Aprili.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma