Kiwanda kikuu cha kuunda magari cha Changchun, China chaanza tena uzalishaji

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 18, 2022

Wafanyakazi wakifanya kazi kwenye eneo la kuunda malori katika Kiwanda cha Kampuni ya kuunda malori FAW Jiefang huko Changchun, Mkoa wa Jilin wa China, Julai 7, 2021. (Xinhua/Zhang Nan)

CHANGCHUN - Viwanda vitano vya Kampuni ya China FAW huko Changchun, mji mkuu wa Mkoa wa Jilin ulioko Kaskazini-Mashariki mwa China, vimeanza uzalishaji hadi kufikia jana Jumapili, na jumla ya wafanyakazi 7,438 wamerejea kazini, serikali ya mji huo imesema.

Wafanyakazi wengine zaidi ya 25,000 kutoka kwa wasambazaji wa vipuri vya magari 276 wa Kampuni ya FAW pia wamerejea kazini.

Shughuli za kawaida za uendeshaji wa viwanda hivyo vitano vya Kampuni ya FAW huko Changchun zilisimamishwa kuanzia Machi 13 kutokana na kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona.

FAW ambayo ni kampuni kuu ya Jilin na sehemu muhimu ya minyororo ya viwanda vya magari ya ndani na kimataifa, iliuza magari milioni 3.5 Mwaka 2021, na mapato yake yalifikia yuan bilioni 707 (kama dola za Kimarekani bilioni 110.6).

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha