Pato la Taifa la China (GDP) laongezeka kwa asilimia 4.8 katika Robo ya Kwanza ya Mwaka 2022

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 18, 2022

Picha iliyopigwa Tarehe 5 Desemba 2021 ikionyesha mandhari ya mawio ya jua kwenye Bandari ya Kimataifa ya Yangpu katika Eneo la Maendeleo ya Kiuchumi wa Yangpu, Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China. (Xinhua/Pu Xiaoxu)

BEIJING - Uchumi wa China ulianza vema katika robo ya kwanza ya Mwaka 2022 licha ya changamoto zinazosababishwa na mazingira magumu ya duniani na kuibuka tena kwa maambukizi ya Virusi vya Korona (UVIKO-19) nchini humo.

Pato la Taifa la China (GDP) liliongezeka kwa asilimia 4.8 katika miezi mitatu ya kwanza ikilinganishwa na mwaka uliopita, na kuongeza kasi ya ukuaji kutoka ongezeko la asilimia 4 katika robo ya nne mwaka jana wa 2021, takwimu kutoka Idara ya Taifa ya Takwimu ya China (NBS) zilionyesha leo Jumatatu.

“Uchumi umeonyesha mwenendo thabiti na kuendelea kuimarika huku China ikisawazisha udhibiti wa janga na maendeleo ya kiuchumi na kijamii” Msemaji wa NBS Fu Linghui amesema katika mkutano na waandishi wa habari.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha