Serikali ya Marekani kupuuza maisha ya binadamu kunafichua unafiki juu ya haki za binadamu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 18, 2022

(Katuni na Ma Hongliang)

Baada ya kuzuka kwa mgogoro wa Ukraine, Serikali ya Marekani, huku ikitoa wito kwa pande husika "kusimamisha vita," hata hivyo iliendelea kumimina mafuta kwenye moto huo kwa njia za haki au chafu.

Mwezi Machi 10, Rais wa Marekani Joe Biden alitia saini mswada wa ufadhili kuwa sheria unaojumuisha msaada wa dola bilioni 13.6 za kimarekani kwa Ukraine. Kwa mujibu wa ripoti ya gazeti la New York Times mapema mwezi Machi, Marekani na washirika wake wa NATO barani Ulaya waliipatia Ukraine silaha zaidi ya 17,000 za kujikinga dhidi ya vifaru ndani ya siku sita tu.

Marekani ilipendekeza Poland kukabidhi ndege zake za aina ya MiG-29 kwa Ukraine na kueleza kuwa Serikali ya Marekani itazingatia kikamilifu kuifidia Poland ikiwa itatekeleza pendekezo lake. Wakati huo huo, Marekani pia ilishirikiana na washirika wake kuiwekea Russia shinikizo la juu, na kuweka maelfu ya vikwazo vikali dhidi ya Russia.

Hatua za Serikali ya Marekani kuwasha moto zaidi na kisha kutia mafuta zaidi kwenye moto huo zimeleta mateso kwa watu wa Ukraine. Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Machi 31 lilisema kwamba zaidi ya watu milioni 4 tayari wamelazimika kuikimbia Ukraine na inakadiriwa watu milioni 6.5 wamelazimika kuyahama makazi yao ndani ya mipaka ya nchi hiyo.

Marekani inadai kwamba vita vya Ukraine vinapaswa kukomeshwa, lakini imeendelea kutoa silaha ili kuwaunga mkono wenzao wa Ukraine. Hii inaonyesha asili ya unafiki wa Wamarekani. Marekani, ambayo inajiita "mtetezi wa amani ya Dunia," badala yake imefichua vigezo vyake viwili na unafiki katika suala la amani ya Dunia.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha