Miji ya Delta ya Mto Yangtze nchini China yaanzisha sera za kusaidia kampuni ndogo

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 19, 2022

Mfanyakazi akifanya kazi katika kampuni ya vipuri vya magari katika Mji wa Anting, eneo la Jiading, huko Shanghai, Mashariki mwa China, Machi 26, 2022. Makampuni nchini China yamekuwa yakidumisha kithabiti uzalishaji chini ya hatua kali za kuzuia na kudhibiti UVIKO-19. (Xinhua/Wang Shujuan)

HANGZHOU - Miji mikubwa inayozunguka Delta ya Mto Yangtze ya China, ambayo ni kitovu cha uchumi wa kibinafsi, imeanzisha hatua kadhaa za kupunguza tatizo la uhaba wa pesa linalozikabili kampuni ndogo na za kati ambalo linasababishwa na kuibuka tena kwa UVIKO-19.

Sera za kifedha kama vile kupunguza kodi na ada, kuongezwa kwa tarehe ya mwisho ya kuwasilisha marejesho ya kodi, na makubaliano ya malipo ya pango zimeanzishwa kwa ajili ya kusaidia makumi ya maelfu ya makampuni ya kibinafsi na wajasiriamali binafsi.

“Sera ziko wazi katika suala la hatua zinazohusu fedha, usimamizi na taarifa kusaidia kufufuka kwa biashara ya rejareja, na kuhusisha idara za serikali zinazowajibika kwa kurahisisha biashara” amesema Ding Zuohong, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Yuexing huko Shanghai.

Makadirio ya awali yanaonyesha kuwa hatua zinazohusiana na kodi zilizochukuliwa na Shanghai zinaweza kupunguza mzigo kwa viwanda na makampuni husika kwa takriban yuan bilioni 140 (karibu dola bilioni 22 za Marekani) Mwaka 2022.

Angalau miji mitatu mikuu katika Delta ya Mto Yangtze - Shanghai, Hangzhou na Suzhou – imeanzisha sera za kuwezesha dhamana ya ufadhili, kutoa ruzuku ya riba, na kuelekeza taasisi za kifedha kutoa mikopo zaidi kwa kampuni ndogo na za kati katika juhudi za kupunguza changamoto za kifedha.

Kunufaika na hatua zinazolengwa kwa sekta ya huduma, ambayo imeathiriwa sana na janga hili, sekta kama vile mikahawa, biashara ya rejareja, utalii, usafirishaji na maonyesho zimeshuhudia kuboreka kwa mazingira ya upatikanaji wa fedha.

Mkoa wa Zhejiang umependekeza kuwa utatoa bure huduma ya upimaji virusi vya Korona kwa wafanyakazi wa biashara ya mikahawa, na kukubali kuchelewa kulipa bima ya ukosefu wa ajira kwa biashara za reja reja zinazostahiki. Hangzhou, mji mkuu wa mkoa huo, umependekeza kuwa itapunguza kodi ya ongezeko la thamani kwa watoa huduma za usafiri wa umma.

Shanghai imehimiza taasisi za dhamana za ufadhili zinazoungwa mkono na serikali kutoa usaidizi wa mikopo kwa mashirika ya usafiri, na imekuwa ikitafakari ruzuku kwa sekta ya maonyesho. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha