Biashara ya nje ya Shanghai yaongezeka kwa asilimia 14.6 katika Robo ya Kwanza ya 2022

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 20, 2022

Picha iliyopigwa Tarehe 15 Aprili 2022 ikionyesha mwonekano wa Bandari ya Yangshan huko Shanghai, Mashariki mwa China. (Xinhua/Ding Ting)

SHANGHAI –Kwa mujibu wa Idara ya Forodha ya Shanghai, Biashara ya nje ya mji huo ulioko Mashariki mwa China ilifikia yuan trilioni 1.01 (kama dola bilioni 158 za Kimarekani) katika robo ya kwanza ya Mwaka 2022.

Idara hiyo imesema kwamba, biashara hiyo na nje iliongezeka kwa asilimia 14.6 kuliko kipindi kama hicho cha mwaka jana.

Kati ya jumla ya kiwango hicho cha biashara, mauzo ya nje yaliongezeka kwa asilimia 23.8 kuliko mwaka jana kwa yuan bilioni 413.5, wakati uagizaji wa bidhaa kutoka nje uliongezeka kwa asilimia 8.9 hadi kufikia yuan bilioni 594.4.

Bidhaa za mitambo na umeme zilichangia asilimia 68.7 ya mauzo ya nje ya mji huo katika robo ya kwanza ya Mwaka 2022, wakati mauzo ya nje ya magari, simu za mkononi, betri za lithiamu-ioni na bidhaa zinazohitaji nguvu kazi kubwa ziliripotiwa kukua pia. Bidhaa za teknolojia ya juu zilikuwa bidhaa kuu za Shanghai zilizoagizwa kutoka nje wakati wa kipindi hicho.

Mshirika mwenzi mkuu wa biashara wa mji wa Shanghai katika robo ya kwanza ya Mwaka 2022 alikuwa Umoja wa Ulaya, huku jumla ya thamani ya biashara kati ya pande hizo mbili ikifikia yuan bilioni 196.2.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha