Mikutano ya kufanya majumuisho na kupongeza Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi na ya Walemavu yafanyika Beijing na Mkoa wa Hebei

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 20, 2022

Aprili 19, Mikutano ya kufanya majumuisho na kupongeza Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi na ya Walemavu ya Beijing imefanyika kwa mfanikio mjini Beijing na Mkoa wa Hebei, China ili kujifunza na kutekeleza kwa kina misingi ya hotuba aliyotoa Rais Xi Jinping wa China kwenye mkutano huo, na kufanya majumuisho kwa pande zote kuhusu uzoefu wa maandalizi ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi, na kupongeza “makundi na Watu waliotoa mchango mkubwa”.

Katibu wa kamati ya Chama ya Mji wa Beijing Bw. Cai Qi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing alisema kuwa, Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi na ya Walemavu ya Beijing imemalizika kwa mafanikio, na kazi za maandalizi ya michezo hiyo zimekuwa kumbukumbu za kufurahisha na hatuwezi kuzisahau. Tunatakiwa kuenzi moyo wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi, na kufanya juhudi zaidi za kusukuma mbele maendeleo ya mji mkuu wa Beijing kwenye mwanzo mpya wa zama mpya, na kujitahidi kutoa majibu mapya mazuri kwa Chama na wananchi.

Katibu wa Kamati ya Chama ya Mkoa wa Hebei ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la Mkoa wa Hebei Bw.Wang Dongfeng alisema, tunatakiwa kuenzi kwa nguvu moyo wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing, kukuza uchumi wa baada ya kumalizika kwa michezo hiyo, kufanya juhudi za kuanzisha hali mpya ya Mkoa wa Hebei unaopendeza, na kujenga mkoa wetu kuwa mkoa wenye nguvu kubwa ya uchumi wa mambo ya kisasa, ili kuukaribisha Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha CPC utakaofanyika kwa mafanikio.

Mikutano hiyo miwili ilitangaza uamuzi kuhusu kupongeza “makundi na watu waliotoa mchango mkubwa” kwenye Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing 2022 na Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Walemavu ya Beijing 2022 katika Mji wa Beijing na Mkoa wa Hebei. Viongozi walioshiriki kwenye mikutano hiyo walitoa tuzo kwa wajumbe wa wale waliopongezwa.

Wajumbe wa “makundi na watu waliotoa mchango mkubwa” walitoa hotuba kwenye mikutano.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha