Kusoma Dunia pamoja na Rais Xi Jinping | Ujamaa

By Zhou Linjia, Song Ge, Zhao Chen, Ma Tianyi (Tovuti ya Gazeti la Umma) April 22, 2022

Leo nitawajulisha kitabu cha Ujamaa kilichokusanya makala mbalimbali zilizoandikwa na Baba wa Taifa la Tanzania Julius Kambarage Nyerere.

Tarehe 25, Machi, 2013, Rais Xi Jinping wa China alipofanya ziara Tanzania alitoa hotuba kwenye Ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere Dar es Salaam akisema, urafiki kati ya Afrika na China una historia ndefu. Kuanzia miaka ya 1950 na 1960, viongozi waasisi wa Jamhuri ya Watu wa China na wa Afrika walianzisha uhusiano kati ya China na Afrika kwa pamoja.

Nyerere ni mmoja wa wawakilishi wa wanasiasa hao.

Tangu kuanzishwa kwa nchi huru ya Tanganyika na baadaye Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais Nyerere ametembelea China mara 13 bila ya kujali safari ndefu, na alikuwa rafiki mkubwa anayejulikana kwa watu wa China. Chuo cha Uongozi cha Julius Nyerere kiliwekwa jiwe la msingi Julai 16, 2018, na kuzinduliwa Februari 23, 2022, ambapo Rais Xi Jinping wa China alituma salamu za pongezi.

Leo maelezo kuhusu kitabu yanaishia hapa. Tunatumai watazamaji wetu mnaweza kupata maarifa fulani mtakapokisoma. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha