Pendekezo la Usalama wa Dunia la Rais Xi linatoa suluhisho na hekima ya China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 24, 2022

Rais Xi Jinping wa China akitoa hotuba kwa njia ya video kwenye ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka 2022 wa Baraza la Asia la Boao, Aprili 21, 2022. (Xinhua/Ding Haitao)

BEIJING – Wataalamu mbalimbali wamesema kwamba, Pendekezo la Usalama wa Dunia la Rais Xi Jinping wa China ni manufaa mengine ya kimataifa kwa umma yanayotolewa na China, kwani linachangia suluhisho na hekima za China katika kutatua changamoto za usalama zinazowakabili wanadamu.

Pendekezo hilo alilotoa Rais Xi siku ya Alhamisi wiki hii alipotoa hotuba kwa njia ya video kwenye ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka 2022 wa Baraza la Asia la Boao (BFA) huko Boao, Mkoa wa Hainan wa China.

“Pendekezo hilo ni faida nyingine ya kimataifa kwa umma inayotolewa na China na sehemu muhimu ya kujenga jumuiya binadamu yenye mustakabali wa pamoja ” amesema Xu Bu, Mkuu wa Taasisi ya masuala ya Kimataifa ya China.

Pendekezo hilo la Usalama wa Dunia linajikita kwenye kujitolea katika maeneo sita:

Kwanza, kuendelea kujitolea kwa wazo la usalama wa pamoja, wa kina, wa ushirikiano na endelevu, na kufanya kazi pamoja kudumisha amani na usalama duniani;

Pili, kuheshimu mamlaka ya nchi na ukamilifu wa eneo la nchi zote, kushikilia kutoingilia mambo ya ndani ya nchi zingine, na kuheshimu machaguo huru ya njia za maendeleo na mifumo ya kijamii yanayofanywa na watu wa nchi mbalimbali;

Tatu, kutii madhumuni na kanuni za Mkataba wa Umoja wa Mataifa, kukataa mawazo ya Vita Baridi, kupinga nadharia na fikra za vitendo vya upande mmoja, na kusema hapana kwa siasa za vikundi na mapambano ya kambi;

Nne, kuchukulia kwa uzito masuala halali ya usalama ya nchi zote, kuzingatia kanuni ya usalama usiogawanyika, kujenga mfumo wa usalama ulio wa uwiano, wenye ufanisi na endelevu, na kupinga kutafuta usalama binafsi kwa gharama ya nchi zingine.

Tano, kusuluhisha kwa njia ya amani migongano na migogoro kati ya nchi kwa njia ya mazungumzo na mashauriano, kuunga mkono juhudi zote zinazosaidia kutatua migogoro kwa amani, kukataa tabia ya ndumilakuwili, na kupinga matumizi mabaya ya vikwazo vya upande mmoja na mamlaka ya mkono mrefu.

Na mwisho, kudumisha usalama katika nyanja za jadi na zisizo za jadi, na kufanya juhudi za pamoja katika mizozo ya kikanda na changamoto za kidunia kama vile ugaidi, mabadiliko ya tabianchi, usalama wa mtandao wa internet na usalama wa viumbe.

Guo Yanjun, Mkurugenzi wa Taasisi ya Masomo ya Asia ya Chuo Kikuu cha Mambo ya Nje cha China, amesema pendekezo hilo litasaidia kujenga maelewano na kukuza mageuzi ya mfumo wa usimamizi wa usalama duniani.

Tofauti na baadhi ya nchi za Magharibi ambazo huangalia maslahi ya upande mmoja kwa usalama wao, Pendekezo la Usalama wa Dunia linazingatia usalama wa pamoja, ambao unasisitiza amani na ushirikiano, amesema Bambang Suryono, Mwenyekiti wa Kituo cha Utafiti na Uvumbuzi cha Jumuiya ya mabingwa washauri ya Asia ya Indonesia.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha