

Lugha Nyingine
Uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Marekani ni wenye manufaa kwa pande zote
CHICAGO – Balozi wa China nchini Marekani Qin Gang Alhamisi wiki hii amesema kwamba, uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Marekani ni wenye manufaa kwa pande zote na kwamba kurejesha uhusiano wa kawaida wa kibiashara kati ya nchi hizo mbili haraka iwezekanavyo ni matarajio ya pamoja ya pande zote mbili.
Qin ametoa kauli hiyo katika Mazungumzo ya Ngazi ya Juu kuhusu kilimo kati China na Marekani kwa Mwaka 2022 yaliyofanyika huko Des Moines, mji mkuu wa jimbo la Iowa la Marekani.
Balozi huyo anatembelea majimbo ya Magharibi-Kati ya Marekani ya Illinois, Iowa na Minnesota, na Des Moines ni kituo chake cha pili katika ziara yake katika Jimbo la Iowa.
Uhusiano wa kilimo kati ya China na Marekani una umuhimu maalumu. Pamoja na janga linaloibuka, kufufuka taratibu kwa uchumi wa Dunia, mabadiliko kwa kasi ya tabianchi na migogoro inayopamba moto ya kikanda, usalama wa chakula limekuwa suala kuu la kivitendo linaloikabili China, Marekani na Dunia yote." Qin amesema.
Qin amesisitiza kuwa China imefanya juhudi kubwa kutekeleza kikamilifu makubaliano ya kibiashara kati ya China na Marekani ya awamu ya kwanza katika miaka miwili iliyopita. "Licha ya janga hili, hatujachukua hatua kali, na hata tumepitisha mchakato maalumu kwa misingi ya soko kwa ushuru wa kukabiliana katika mazao ya maharage ya soya, nafaka, nyama, bidhaa za majini na matunda kutoka Marekani. Hii inaonyesha kikamilifu uaminifu wetu na nia njema," amesema.
Qin huku akinukuu ripoti ya hivi majuzi ya Mauzo ya Nje ya Marekani iliyotolewa na Baraza la Biashara kati ya China na Marekani amesema, wakati China ikitekeleza makubaliano hayo ya kibiashara ya awamu ya kwanza, wakulima wa Marekani wameuza nje kwa zaidi ya mabilioni ya dola mbegu za mafuta na nafaka na zaidi ya dola bilioni moja zaidi katika bidhaa za nyama, jambo ambalo limeboresha ustawi wa wakulima katika kitovu cha Marekani.
“Wakati huo huo, ukuaji wa mauzo haya ya nje unatoa maelfu ya nafasi za ajira kwa zaidi ya wilaya kumi na mbili za kibunge za Marekani” ameongeza.
Mazungumzo ya Ngazi ya Juu kuhusu kilimo kati China na Marekani kwa Mwaka 2022 yameandaliwa kwa pamoja na Ubalozi wa China nchini Marekani, Shirika la Heartland la Marekani, na Shirika la mabadilishano ya kilimo la kimataifa la China, na kuhudhuriwa na maofisa wa kilimo, viongozi wa vyama vya kilimo na makampuni kutoka China na Marekani zaidi ya 500 kwa ana kwa ana au mtandaoni.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma