Mtaalamu Mkuu asisitiza kuwa sera ya China ya maambukizi sifuri ya UVIKO inalenga milipuko na siyo maambukizi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 26, 2022

Picha iliyopigwa Aprili 23, 2022 ikionyesha tangi la oksijeni katika hospitali ya muda huko Shanghai. (Xinhua/Yang Youzong)

BEIJING - Mtaalamu wa magonjwa ya mlipuko wa China amesisitiza kwamba sera madhubuti ya China ya ‘maambukizi sifuri ya UVIKO’ inalenga kutokomeza milipuko ya maambukizi ya virusi vya Korona, na hailengi kuondoa maambukizi ya mtu binafsi.

"Kiini cha sera madhubuti ya maambukizi sifuri ya UVIKO ni kutambua mapema maambukizi ya virusi na kuyadhibiti kwa haraka ili kukomesha kuenea kwa virusi katika jamii na kulinda afya na maisha ya watu kwa kiwango kikubwa kadiri iwezekanavyo," Liang Wannian, mkuu wa jopo la wataalam wa kukabiliana na UVIKO-19 lililo chini ya Kamati ya Taifa ya Afya ya China, ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua katika mahojiano ya hivi karibuni.

Akifafanua dhana hiyo, Liang amesema "madhubuti" inamaanisha kuwa, ingawa haiwezi kuhakikishwa kuwa hakuna mtu atakayeambukizwa virusi vya Korona ndani ya muda mfupi, China inaweza kutambua kwa haraka na kudhibiti milipuko mara tu inapobainika ili kuzuia virusi kusababisha madhara makubwa kwa idadi kubwa ya watu.

“Kwa sasa, sera ya nchi ya "maambukizi sifuri ya UVIKO" inahusisha mchakato wa kutoa nguvu kubwa kwa kuzuia kuenea kwa milipuko, maambukizi endelevu kwenye maeneo ya makazi, na kuibuka tena kwa maambukizi kwa kiwango kikubwa, na hailengi kutokomeza virusi vya Korona vya aina mpya” amesisitiza.

China inashindana na wakati ili kudhibiti kuongezeka kwa maambukizi ya virusi vya Korona yaliyoanza Mwezi Machi Mwaka huu. China Bara mwishoni mwa wiki iliyopita siku ya Jumamosi ililiripoti watu walioambukizwa virusi vya korona walifikia 21,796, kutoka watu 24,326 walioripotiwa siku ya Ijumaa.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha