China kushirikiana na jumuiya ya kimataifa kutekeleza Pendekezo la Usalama wa Dunia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 26, 2022

BEIJING - Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi amesema kwamba, China iko tayari kushirikiana na jumuiya ya kimataifa katika kuhakikisha Pendekezo la Usalama wa Dunia linakita mizizi na kuchanua maua ili kuifanya Dunia iwe na amani, usalama na ustawi zaidi.

"Pendekezo hilo, lililotolewa na Rais wa China Xi Jinping, linachangia hekima ya China katika kushughulikia nakisi ya amani ya binadamu na kutoa suluhisho ya China ili kukabiliana na changamoto za usalama wa Dunia," Wang amesema katika makala iliyochapishwa Jumapili ya wiki kwenye Gazeti la People's Daily la China.

Wang amesema, pendekezo hilo linaendana na mahitaji ya dharura ya jumuiya ya kimataifa ya kudumisha amani ya Dunia na kuzuia migogoro na vita, linaendana na utafutaji wa pamoja wa nchi zote duniani kuunga mkono mfumo wa pande nyingi na kudumisha mshikamano wa kimataifa, na kufuata matakwa ya pamoja ya watu wa nchi mbalimbali ya kushinda matatizo na kujenga Dunia bora baada ya janga la virusi vya Korona.

Pendekezo la Usalama wa Dunia linapendekeza kushikilia ahadi katika maeneo sita, ambayo ni: kushikilia wazo la usalama wa pamoja, wa jumla, wa ushirikiano na endelevu; kuheshimu mamlaka ya nchi na ukamilifu wa ardhi ya nchi zote; kushikilia nia na kanuni za “ Katiba ya Umoja wa Mataifa”; kujitolea kutatua kwa njia ya amani migongano na migogoro kati ya nchi kupitia mazungumzo na mashauriano; kuendelea kujitolea kudumisha usalama katika nyanja za jadi na zisizo za jadi.

Wang ameongeza kuwa pendekezo hilo pia limekita mizizi katika desturi na hekima ya kidiplomasia yenye umaalumu wa China. China ikiwa nchi kubwa inayowajibika siku zote imekuwa ikishikilia bendera ya amani, maendeleo na ushirikiano wa kunufaishana kati ya pande zote, ikitoa mchango kwa ajili ya kulinda amani na usalama duniani, na kuwa nchi kubwa ya mfano. Wang amesema kuwa, China iko tayari kushikana mikono na nchi zote zinazopenda amani na maendeleo na watu wote ili kutekeleza Pendekezo la Usalama wa Dunia, kufuata njia ya kudumu ya amani na usalama wa Dunia nzima, na kuwa na nguvu kubwa ya pamoja ili kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha