China kuongeza zaidi uwezo wa ununuzi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 26, 2022

Mkazi akinunua vitu kwenye duka huko Yinchuan, Ningxia, China Tarehe 23, Oktoba, 2021. (Picha/Xinhua)

Jumatatu wiki hii China ilitoa mwongozo wa kuongeza zaidi uwezo wa ununuzi wa taifa, pamoja na hatua za kina za kutatua matatizo ya muda mfupi na kustawisha uhai wa ununuzi wa kipindi kirefu.

China inapanga kujenga kundi la mabohari kwenye vitongoji vya miji mikubwa na ya kati ili kuhakikisha kuna ugavi wa kutosha wa mahitaji muhimu ya kila siku wakati wa dharura.

Mwongozo huo pia umebainisha hatua nyingine za kukabiliana na athari za maambukizi ya virusi vya korona na kuhimiza ufufukaji wa ununuzi wa bidhaa.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha