Wizara ya Biashara hina yaongeza utoaji wa mahitaji muhimu kwa mikoa inayoathiriwa na kuibuka tena kwa Korona

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 29, 2022

Mwananchi akichagua mboga kwenye moja ya supamaketi katika eneo la Haidian la Beijing, China, Aprili 26, 2022. (Xinhua/Ren Chao)

BEIJING - Wizara ya Biashara ya China imekuwa ikifanya jitihada nyingi kuongeza utoaji wa mahitaji muhimu ya kila siku kwa mikoa inayokabiliwa na kuibuka tena kwa maambukizi ya virusi vya Korona (UVIKO-19), Wizara hiyo imesema Alhamisi wiki hii.

“Wizara imekuwa ikisafirisha bidhaa kutoka maeneo mbalimbali hadi katika mikoa iliyoathiriwa ili kuhakikisha upatikanaji wa mahitaji muhimu ya kila siku” Msemaji wa wizara hiyo Gao Feng amesema katika mkutano na waandishi wa habari.

Hadi kufikia Jumatano, maeneo 12 ya ngazi ya mkoa, ikiwa ni pamoja na Mongolia ya Ndani, Liaoning, Zhejiang na Fujian, yalikuwa yameipatia Shanghai tani 27,808 za mboga, tani 850 za mchele na unga, tani 500 za nyama na mayai, na tani 6,180 za tambi.

Jana Alhamisi, Kamati ya Afya ya Mji wa Shaghai ilisema kwamba mji huo uliripoti watu waliothibitishwa kuambukizwa virusi vya Korona walifikia karibu 1,292 na wengine 9,330 walioambukizwa ni wasioonesha dalili mbaya.

“Ili kusaidia maeneo yanayokabiliwa na hatua kali za kuzuia maambukizi ya virusi vya Korona, wizara imeongeza usafirishaji wa mazao ya kilimo kutoka maeneo jirani ya ngazi ya mkoa” Gao amesema.

Ameongeza kwamba, wakati likizo ya Siku ya Wafanyakazi inakaribia, wizara imesisitiza serikali za mikoa nchini China kuongeza zaidi utoaji wa mahitaji ya kila siku ili kukidhi mahitaji muhimu ya wakazi wakati wa likizo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha