Uchumi wa Marekani wadorora katika Robo ya Kwanza ya Mwaka 2022

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 29, 2022

Watalii wakinunua bidhaa karibu na Maonyesho ya Mifugo ya Houston ya 2022 huko Houston, Texas, Marekani, Februari 28, 2022. (Xinhua/Xu Jianmei)

WASHINGTON - Uchumi wa Marekani ulidorora kwa asilimia 1.4 katika robo ya kwanza mwaka huu huku kukiwa na ongezeko la maambukizi ya virusi vya Korona aina ya Omicron na kupanda kwa mfumuko wa bei, hali inayoibua hofu ya kuzorota kwa uchumi.

Takwimu hizi mpya zinaashiria uchumi wa Marekani kudorora kwa mara ya kwanza tangu janga la UVIKO-19 lisababishe uchumi kudorora sana mapema Mwaka 2020.

"Tutakuwa na mdororo wa kiuchumi. Hakuna ambacho ni uhakika katika maisha ya kiuchumi, lakini hilo ni jambo la hakika," Gary Hufbauer, afisa wa zamani Wizara ya Fedha ya Marekani na mfanyakazi mwandamizi asiye mkazi katika Taasisi ya Uchumi wa Kimataifa ya Peterson, ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua.

Kwa mujibu wa takwimu kutoka Wizara ya Kazi ya Marekani, kiwango cha bei ya wanunuzi katika Mwezi Machi kilipanda kwa asilimia 8.5 kutoka mwaka uliotangulia, ikiwa ni ongezeko kubwa zaidi la miezi 12 tangu kipindi kilichoishia Desemba 1981.

Mteja akichagua bidhaa za vyakula kwenye supamaketi huko Millbrae, Marekani, Machi 10, 2022. (Picha na Li Jianguo/Xinhua)

Desmond Lachman, Mtaalamu Mwandamizi katika Taasisi ya Biashara ya Marekani na afisa wa zamani katika Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), pia ameelezea uwezekano wa mdororo wa kiuchumi nchini Marekani, akisema kuwa sababu nyingine ya kukatisha tamaa ni mabadiliko ya hivi majuzi katika mkondo wa upatikanaji wa faida.

"Labda kinachosumbua zaidi ni kwamba sera zinazoimarishwa zaidi za Benki Kuu huenda zitaleta uwezekano wa kudorora kwa madeni ya mitaji na soko la nyumba," Lachman ameongeza.

Wachambuzi mara nyingi huhusisha kushuka kwa uchumi na kupungua kwa pato la taifa (GDP) kwa robo mbili mfululizo za mwaka. Baadhi ya wataalamu wa uchumi, wakati huo huo, wametoa kauli zenye matumaini zaidi, wakisema kwamba kudhoofika kwa uchumi kunaweza kuzidishwa na takwimu ya Pato la Taifa.

Mwenyekiti wa Benki Kuu ya Marekani Jerome Powell akitoa ushahidi mbele ya Kamati ya Seneti ya Benki mjini Washington, D.C., Marekani, Januari 11, 2022. (Brendan Smialowski/Pool kupitia Xinhua)

Hata Mwenyekiti wa Benki Kuu ya Marekani Jerome Powell, ambaye alisema kuwa kutua laini, au angalau hatua lainishi imekuwa jambo la kawaida katika historia ya mfumo wa fedha wa Marekani, amebainisha kuwa hakuna mtu anayetarajia kwamba kuleta unafuu wa mikopo itakuwa moja kwa moja au rahisi katika mazingira ya sasa.

"Itakuwa na changamoto nyingi." Powell amesema. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha