Ripoti yaonesha wanunuzi bidhaa wa China wana matumaini zaidi kuhusu siku zijazo

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 04, 2022

BEIJING - Ripoti iliyochapishwa na Kampuni ya Ushauri ya Kimataifa ya Ernst & Young (EY) inaonesha kwamba, wanunuzi bidhaa wa China wana matumaini zaidi kuhusu siku zijazo tofauti na kupungua kwa imani miongoni mwa wanunuzi bidhaa duniani

“Takribani asilimia 60 ya watu waliohojiwa kutoka China waliamini kuwa uwezo wao wa kifedha utaimarika katika mwaka ujao, ikiwa ni zaidi ya wastani wa kimataifa wa asilimia 48” Kwa mujibu wa ripoti ya hivi punde ya Ernst & Young kuhusu Kielezo cha Wanunuzi wa Bidhaa katika siku zijazo ambayo inafuatilia mabadiliko ya hisia na tabia za wanunuzi bidhaa katika masoko mbalimbali duniani huku wanunuzi wa bidhaa18,000 wakihojiwa na kutafitiwa kote duniani.

Takwimu kutoka kampuni hiyo zinaonesha kwamba, asilimia 43 ya wanunuzi bidhaa wa China wanasema hali yao ya kifedha kwa sasa imeimarika kutokana na kupunguza matumizi kwa kiasi, ambayo ni asilimia 9 zaidi kuliko wastani wa Dunia.

“Wakati mabadiliko ya tabianchi na maendeleo endelevu yakiendelea kuvutia tahadhari duniani, watumiaji wengi zaidi wanasema wanafahamu athari za tabia zao za manunuzi kwenye mazingira na wanajumuisha hilo kuwa moja ya sababu kuu katika kuzingatia manunuzi yao” inasema ripoti hiyo.

Takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 32 ya watu waliohojiwa wa China walisema wataweka kipaumbele kwa uendelevu na mazingira katika kununua bidhaa, zaidi ya wastani wa Dunia wa asilimia 26.

"Chini ya mwongozo wa 'kilele cha kaboni ifikapo Mwaka 2030 na usawazishaji wa kaboni ifikapo Mwaka 2060’, wanunuzi bidhaa wa China wameonyesha uelewa wa kiwango cha juu kuhusu maendeleo endelevu, wakianza kufikiria upya tabia zao za manunuzi na kufuata uendelevu," anasema Denis Cheng, Kiongozi wa Kampuni ya Ernst & Young anayeshughulikia Sekta ya Wanunuzi bidhaa nchini China.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha