China yanunua zaidi ya nusu ya magari yanayotumia nishati ya umeme duniani katika robo ya kwanza ya Mwaka 2022

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 05, 2022

Picha ikionesha gari linalotumika umeme la i3s la BMW kwenye maonesho ya magari ya kimataifa ya Munich, Ujerumani, Septemba 7, 2021. (Picha/Xinhua)

BERLIN - Kwa mujibu wa ripoti iliyolewa na kampuni ya ukaguzi wa mahesabu na huduma za ushauri PwC Strategy & (Ujerumani) siku ya Jumatano wiki hii, magari mawili kati ya matatu yanayotumia betri za umeme (BEVs) yaliyouzwa duniani kote katika robo ya kwanza (Q1) ya Mwaka 2022 yalinunuliwa na watu kutoka China.

Soko la China la BEV limeongezeka zaidi ya mara mbili kuzidi mwaka jana, na kufikia idadi ya magari milioni moja katika robo ya kwanza ya Mwaka 2022, kwa mujibu wa ripoti hiyo. "Kiwango cha ukuaji nchini China kiliendelea kushinda masoko mengine muhimu ya magari yanayotumia nishati ya umeme."

Ripoti hiyo inaonesha kwamba, Ujerumani imeendelea kuwa soko kubwa zaidi la BEV barani Ulaya kwa idadi ya magari yaliyouzwa, lakini soko la hisa la BEV lilikuwa kubwa zaidi nchini Uingereza kwa sababu ya upatikanaji mkubwa wa bidhaa. Katika masoko matano ya juu ya Ulaya, mauzo ya BEV yalifikia magari 210,940 ambayo yaliongezeka kwa asilimia 46 kuzidi mwaka jana.

“Ndani ya mwaka mmoja, watengenezaji magari wa Ujerumani walikuwa wameongeza maradufu hisa zao katika soko la China la BEV hadi kufikia asilimia 4” Mtaalam wa PwC Felix Kuhnert ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua Jumatano wiki hii.

Mauzo ya BEV duniani katika robo hiyo ya kwanza yaliongezeka kwa asilimia 107 kuzidi robo ya kwanza ya mwaka jana. "Mengi ya magari yaliyouzwa yalinunuliwa nchini China," PwC Strategy& imesema. Wafanyabiashara wa magari wa Ujerumani BMW, wametangaza kwamba mauzo yake ya BEV nchini China yameongezeka mara tatu ikilinganishwa na mwaka jana.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha