Msaada wa vitabu wa China kwa shule ya Madagaska kuhumiza mabadilishano ya kitamaduni

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 06, 2022

Balozi wa China nchini Madagaska Guo Xiaomei (Kulia) na wageni wengine wakionekana wakati wa hafla ya uzinduzi wa chumba cha kujisomea katika shule ya Le Petit Nid huko Antananarivo, Madagaska, Mei 5, 2022. Serikali ya China Alhamisi wiki imetoa karibu vitabu 3,000 vya Kichina na vya lugha mbili za Kichina na Kifaransa kwa shule hiyo. (Xinhua/Sitraka Rajaonarison)

ANTANANARIVO - Serikali ya China Alhamisi wiki hii imetoa vitabu karibu 3,000 vya Kichina na vya lugha mbili za Kichina na Kifaransa kwa shule huko Madagaska.

"China inafurahi kutoa vitabu 3,000 vya lugha ya Kichina na vya lugha mbili za Kichina na Kifaransa kwa ajili ya chumba hiki cha kujisomea," Guo Xiaomei, Balozi wa China nchini Madagaska, amesema wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi wa chumba hicho katika shule ya Le Petit Nid huko Antananarivo.

Guo amesema mchango huo ni pamoja na vitabu kwa ajili ya watoto vilivyo na maudhui yanayohusu fasihi nne kuu za Kichina, pamoja na utamaduni, desturi za jadi za China.

"Nina imani kwamba vitabu hivi vitatoa dirisha la kufahamu China kwa marafiki wanafunzi wa shule," Guo amesema, akiongeza kuwa anatumai vijana wa Madagascar watafurahia kusoma, kupata maarifa mapya, na kupanua maono yao katika chumba hicho cha kujisomea.

Ratsimisetra Felambohangy, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu ya Madagascar amesema kuwa vitabu, viwe vya maandishi au vya kielektroniki, vinawakilisha mojawapo ya zana za maarifa zinazopendekezwa zaidi.

"Tuna imani kwamba, kutokana na msaada wako, zana za elimu zinazopatikana kwa watoto wa shule ya Le Petit Nid zitawaruhusu kufungua madirisha mengine, haswa ya China," ameongeza.

Wakati huo huo, Ramahafalisoa Sahoby Mampionona, Mkurugenzi Mtendaji wa Ecole Le Petit Nid, ameelezea msaada wa vitabu vilivyotolewa na China ni kama "ishara ya kiungwana kwani vitabu vinaleta hekima."

"Kujifunza lugha ni kuhusu kubadilishana maneno na utamaduni," amesema.

Ikiwa imeanzishwa Mwaka 1987, Shule ya Le Petit Nid inatoa elimu ya ngazi ya chekechea, msingi, sekondari na sekondari ya upili. Masomo ya lugha ya Kichina yamekuwa yakifundishwa katika shule hiyo tangu Mwaka 2013, wakati Darasa la Confucius lilifunguliwa shuleni hapo Mwaka 2017.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha