

Lugha Nyingine
China yasema itashinda vita dhidi ya UVIKO-19 huko Shanghai kwa sera za kudhibiti janga zilizojaribiwa kwa wakati
Picha iliyopigwa Aprili 11, 2022 ikionyesha eneo la Pudong katika Mji wa Shanghai nchini China. (Xinhua/Chen Jianli)
BEIJING – Mkutano wa uongozi wa juu wa China uliofanyika Alhamisi wiki hii umesema kwamba, nchi hiyo hakika itashinda vita dhidi ya janga la virusi vya Korona (UVIKO-19) kwa kutumia sera zake za kisayansi na madhubuti za kudhibiti janga ambazo zitastahimili muda mrefu.
Mkutano wa Kamati ya Kudumu ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) umeongozwa na Xi Jinping, ambaye ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya CPC.
Mkutano huo umechambua na kutathmini hali ya sasa ya kuzuia na kudhibiti mlipuko wa virusi vya Korona, kufahamishwa vipaumbele na kupanga mipango kazi husika.
Mkutano huo umesema tangu Machi mwaka huu, China imestahimili mtihani wa kudhibiti UVIKO-19, ugonjwa ambao ni changamoto zaidi tangu vita dhidi ya janga la Wuhan, na imepata maendeleo mazuri kutokana na juhudi za pamoja za watu wote nchini.
Kwa mujibu wa mkutano huo ambao pia ulionya juu ya hali ya kulegalega kwa juhudi za kudhibiti, wakati janga hilo bado linaenea kote duniani na ugonjwa wa virusi vya Korona ukiendelea kubadilika, bado kuna hali ya kutokuwa na uhakika juu ya jinsi janga hilo litakavyokua.
"Kulegalega bila shaka kutasababisha idadi kubwa ya watu walioambukizwa virusi, wagonjwa wengi mahututi na vifo, na kuathiri vibaya maendeleo ya kiuchumi na kijamii na maisha ya watu na afya," mkutano huo umesema.
Mkutano huo umesisitiza umuhimu wa kufuata bila kuyumbayumba sera thabiti ya maambukizi sifuri ya UVIKO na kupambana kwa uthabiti na majaribio yoyote ya kupotosha, kushuku au kutupilia mbali sera ya China ya kupambana na UVIKO.
Udhibiti wa UVIKO-19 uko katika hatua muhimu, mkutano umesema, huku ukitoa wito kwa kamati za Chama na serikali katika ngazi zote kubaki na ujasiri na kukuza moyo wa mapambano ili kujenga ulinzi thabiti dhidi ya janga hili.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma