Beijing bado iko kipindi muhimu cha mapambano dhidi ya Maambukizi ya virusi vya korona

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 09, 2022

Mhudumu wa afya akijiandaa kwa kuchukua sampuli kwa mkazi kwa ajili ya kupima virusi vya korona kwenye kituo cha upimaji mjini Beijing, Mei 7, 2022. (Picha/Xinhua)

Ofisa mmoja wa afya wa Beijing alisema, mapambano ya Beijing dhidi ya maambukizi mapya ya virusi vya korona bado yako kipindi muhimu.

Naibu Mkurugenzi wa Kituo na kukinga na kudhibiti wa maradhi cha Beijing Pang Xinghuo Jumamosi ya wiki iliyopita kwenye mkutano na waandishi wa Habari alisema, katika masaa 24 yaliyopita toka Jumamosi ya wiki iliyopita saa 9 mchana kwa saa za Beijing, Beijing imeripoti watu wapya 78 walioambukizwa virusi vya korona.

Pang alisema, kati ya watu hao, watu 70 ni wa maeneo ya kudhibitiwa, na wengi wawili waligunduliwa kwenye upimaji wa eneo la makazi. Katika maambukizi yaliyoanzia tarehe 22, Aprili, mji huu ulirekodi watu wapya 688 waliothibitishwa kuambukizwa virusi vya korona.

Pang alisema, kwa kuwa minyororo ya maambukizi ya virusi bado haijakatwa kabisa kwenye maeneo ya makazi, mji wa Beijing unatakiwa kuchukua hatua za kasi zaidi na kali zaidi za kuzuia maambukizi ya virusi vya korona.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha