Mamlaka ya hifadhi za taifa Tanzania yaanzisha utalii wa kupanda baiskeli kwenye Mlima Meru

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 09, 2022

DAR ES SALAAM – Mamlaka ya Hifadhi za Taifa ya Tanzania (TANAPA) Jumapili wiki hii imeanzisha utalii wa kupanda baiskeli, huku waendesha baiskeli 27 wakishiriki kwenye utalii wa kupanda Mlima Meru wenye urefu wa Mita 4,566 ulioko Kaskazini mwa nchi hiyo.

Waendesha baiskeli 27, wakiwemo wafanyabiashara wa utalii na watalii, walianza jaribio lao la kuupanda mlima huo wa tano kwa urefu wake barani Afrika, zoezi ambalo litawachukua siku tatu kwa kupanda na kushuka.

Akizungumza chini ya Mlima Meru, Kamishna mhifadhi wa Hifadhi ya Taifa ya Arusha, Albert Mziray, amesema utalii wa kupanda baiskeli katika mlima huo ni dhana mpya yenye uwezo wa kuvutia wageni na watalii wengi katika eneo hilo.

Ofisa Mwandamizi wa TANAPA, Catherine Mbena, amesema TANAPA itaongeza shughuli za utalii ili kuwawezesha watalii watembelee katika maeneo yenye vivutio mbalimbali.

Thad Peterson, kiongozi wa msafara huo, amesema watalii sasa wanakuwa na utambuzi zaidi na wanataka mazoezi zaidi hata wakati wa utalii. Peterson amesema, dhamira hiyo imeweka msingi wa kupata watalii wengi zaidi wa kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Arusha, ambapo wataweza kutembelea pia katika maeneo yenye wanyamapori na mimeapori na vivutio mbalimbali.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha