Sura ya Marekani katika mgogoro kati ya Ukraine-Russia: Marekani yanufaika kutoka kwa mgogoro huku Ulaya ukikula hasara

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 10, 2022

Jumuiya ya NATO inayoongozwa na Marekani inayopanua tena na tena kwa Mashariki ni moja ya sababu ya mgogoro kati ya Russia na Ukraine, lakini sehemu kubwa ya hasara inayoletwa na mgogoro inabebwa na Ulaya.

Tarehe 24, Machi, mwaka huu, rais Joe Biden wa Marekani alipohutubia mkutano wa kilele wa G7 alisema, “NATO haijawahi kuwa mshikamano wa namna hii ya hivi sasa.” Bila shaka maneno hayo “yaliteka nyara” Ulaya kupanda gari la vita la Marekani, na kuilazimisha ifuate hatua za kuweka vikwazo za Marekani, na kuzilipa.

Kutokana na vikwazo vikubwa dhidi ya Russia, viwango vingi vya uchumi vya Ulaya vimeathiriwa vibaya. Mjumbe wa mambo ya uchumi wa Kamati ya Umoja wa Ulaya Bw. Gentiloni aliwahi kusema, baada ya kulipuka kwa mgogoro kati ya Russia na Ukraine, bei za bidhaa kubwa zimepandishwa juu kwa kasi zikipandisha mfumuko wa bei hadi kiwango cha juu zaidi, kukatika kwa mawasiliano ya biashara kumeongeza shinikizo la minyororo ya ugavi, matumaini ya wanunuzi yamepungua sana, uchumi wa Ulaya utaathiriwa vibaya kwa muda mrefu sana. Na suala la wakimbizi lililosababishwa moja kwa moja na vita limeleta shinikizo kubwa kwa nchi za Ulaya. Tarehe 20, Aprili, shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) lilisema, hivi sasa wakimbizi zaidi ya milioni 5 wamemiminikia nchi jirani za Ulaya, na hali hiyo imesababisha msukosuko wa wakimbizi ambao haukutokea hapo kabla.

Lakini Marekani ikiwa mchochezi wa mgogoro kati ya Russia na Ukraine imenufaika kutoka kwa mgogoro huo. Katika soko la mambo ya fedha, soko la hisa limebwagwa chini , thamani ya Euro imepungua kwa kiasi kikubwa, huku mitaji mingi ya Ulaya ya kuepusha hatari imeingia Marekani; kwa upande wa suala la wakimbizi, katika miezi mitatu iliyopita Marekani iliwapokea wakimbizi 12 tu kutoka Ukraine, na bado wapo wakimbizi wengi kutoka Ukraine wanaong’ang’ania kwenye mpaka kati ya Marekani na Mexico; Tangu mgogoro ulipoanza, thamani ya hisa za kampuni kubwa za Marekani za viwanda vya silaha imepandishwa kwa kasi, na kampuni hizo zimetajirika kwa sababu ya vita hivyo.

Katika mgogoro kati ya Russia na Ukraine, nani amenufaika na nani amekula hasara? Ukweli unadhihirika bila ya kueleza.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha