Biashara ya nje ya China yaonyesha ustahimilivu wakati wa kukumbwa na janga la UVIKO-19

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 10, 2022

(Picha inatoka Xinhua.)

BEIJING - Biashara ya nje ya China ilidumisha uthabiti na kasi ya ukuaji katika miezi minne ya kwanza ya Mwaka 2022 katika wakati wa kukumbwa na maambukizi ya virusi vya Korona katika maeneo mengi ya ngazi ya mikoa.

Idara Kuu ya Forodha ya China imesema jana Jumatatu kwamba, katika kipindi cha Januari-Aprili, jumla ya uagizaji na mauzo ya bidhaa ya nje ya China iliongezeka kwa asilimia 7.9 kuliko mwaka jana kipindi kama hicho hadi kufikia fedha za RMB Yuan trilioni 12.58.

Kwa mahesabu ya dola ya Marekani, jumla ya biashara ya nje ya China ilifikia dola za Marekani trilioni 1.98 katika kipindi hicho, ikiwa ni ongezeko la asilimia 10.1 kuliko mwaka wa jana.

Takwimu zinaonesha kwamba, mauzo ya nje yaliongezeka kwa asilimia 10.3 kuliko mwaka jana hadi kufikia Yuan trilioni 6.97, wakati uagizaji wa bidhaa kutoka nje uliongezeka kwa asilimia 5 hadi kufikia Yuan trilioni 5.61 katika kipindi hicho, na thamani ya urari ya biashara ilifikia Yuan trilioni 1.36.

Biashara ya China na washirika wenzi wake wakuu watatu wa kibiashara -- Umoja wa nchi za Kusini-Mashariki za Asia, Umoja wa Ulaya, na Marekani ilidumisha kasi nzuri ya ukuaji.

Takwimu za forodha zinaonesha kwamba, katika kipindi hicho, ongezeko la thamani ya biashara ya China na washirika hawa watatu wa kibiashara lilifikia asilimia 7.2, asilimia 6.8 na asilimia 8.7.

Mashirika ya kibinafsi yalishuhudia ukuaji wa haraka huku uagizaji na mauzo yao ya nje ya bidhaa yakiongezeka kwa asilimia 11 hadi kufikia yuan trilioni 6.1 katika miezi minne ya kwanza, ikichukua asilimia 48.5 ya jumla ya biashara yote ya China

Hata hivyo, kwa ufuatiliaji wa biashara ya kila mwezi ya China, biashara ya nje ya China ilipungua kwa asilimia 1.5 mwezi uliopita, na mauzo ya nje yamepungua kwa asilimia 0.6 na uagizaji wa bidhaa kutoka nje ulipungua kwa asilimia 2.5.

"Biashara ya nje ya China inakabiliwa na mazingira magumu na yenye changamoto ya maendeleo," anasema Zhuang Rui, profesa katika Chuo Kikuu cha Biashara ya Kimataifa na Uchumi cha China. Amehusisha kushuka kwa ukuaji wa biashara ya nje na mambo yasiyotarajiwa kama vile janga la UVIKO-19 na mgogoro kati ya Russia na Ukraine.

"Kuibuka tena kwa janga hilo katika miji mikubwa ya usafirishaji bidhaa kumeathiri moja kwa moja uuzaji wa bidhaa nje," wachambuzi wa Taasisi ya Dhamana ya Hongta wamesema katika ripoti yao ya utafiti.

Hata hivyo utafiti huo umeeleza kwamba usumbufu unaosababishwa na maambukizi ya virusi vya Korona kwa biashara ya nje ya China utapungua kwani janga hilo linadhibitiwa polepole na minyororo ya usambazaji wa ndani na minyororo ya viwandani inarejea hali ya kawaida.

Siku ya Alhamisi, Waziri Mkuu wa China Li Keqiang alitaja hatua za kisera za kuleta utulivu wa biashara ya nje huku kukiwa na jitihada za kulainisha minyororo ya viwanda na ugavi wakati akiongoza mkutano wa utendaji wa Baraza la Serikali la China.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha