

Lugha Nyingine
Maonyesho ya utamaduni wa China yafanyika katika chuo kikuu cha Ghana ili kuimarisha uhusiano wa kirafiki
Watu wakishiriki katika mchezo wa kutumia vijiti vya kulia chakula ili kuokota maharagwe wakati wa maonyesho ya utamaduni wa China huko Accra, mji mkuu wa Ghana, Mei 8, 2022. Taasisi ya Confucius katika Chuo Kikuu cha Ghana Jumapili wiki iliyopita iliandaa maonyesho ya utamaduni wa China kwa hadhira ya Ghana ili kukuza uhusiano wa kitamaduni kati ya watu wa nchi hizo mbili. (Xinhua/Xu Zheng)
ACCRA - Taasisi ya Confucius katika Chuo Kikuu cha Ghana Jumapili wiki iliyopita iliandaa maonyesho ya utamaduni wa China kwa hadhira ya Ghana ili kukuza uhusiano wa kitamaduni kati ya watu wa nchi hizo mbili.
Baadhi ya wanafunzi na wafanyakazi wa Taasisi ya Confucius waliandaa maonyesho hayo, ikiwa ni pamoja na ngoma ya mapanga, Opera ya Sichuan na nyimbo za Kichina.
Taasisi hiyo pia iliandaa baadhi ya michezo kama vile kutumia vijiti vya kulia chakula kuokota maharagwe. Wale walioshinda michezo hiyo walipokea mafundo ya Kichina kama zawadi.
Mkuu wa Taasisi ya Confucius kutoka China Chu Beijuan amesema tukio hilo ni sehemu ya juhudi za kuimarisha uhusiano wa kirafiki kati ya China na Ghana.
"Tutajumuisha sanaa za maandishi ya kichina, sanaa za Kongfu, na aina zingine za utamaduni wa Kichina katika kozi zetu za lugha ya Kichina, kwa sababu tunataka watu wengi waelewe lugha na utamaduni wa Kichina," ameongeza.
Henry Nii Adjiri Quarcoopome, mwanafunzi kutoka Taasisi ya Confucius katika Chuo Kikuu cha Ghana, ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua kwamba kujifunza lugha ya Kichina kumekuwa jambo la lazima kwa wanafunzi wanaotafuta ajira katika soko la ajira baada ya kuhitimu.
"Taratibu, tutakuwa tukishirikiana na watu wa China kwa ajili ya shughuli za za ujenzi wa miundombinu yetu na shughuli nyingine za kiuchumi," Quarcoopome amesema.
Pascalina Arthur, mwanafunzi mwingine, amesema Taasisi ya Confucius imekuwa ikiziba pengo la kitamaduni kati ya Ghana na China.
"Mtazamo wa kirafiki wa walimu wa lugha ya Kichina huongeza hamu ya wanafunzi katika lugha hiyo na kuwafanya wazidi kuipenda lugha ya Kichina," amesema.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma