Juzuu ya Kwanza na ya Pili za “Mkusanyiko wa Hotuba za Xi Jinping Kuhusu Mambo ya Kidiplomasia ” zachapishwa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 12, 2022

Juzuu ya kwanza na ya pili za “Mkusanyiko wa Hotuba za Xi Jinping Kuhusu Mambo ya Kidiplomasia ” zilizohaririwa na Taasisi ya historia ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na nyaraka muhimu za Kamati Kuu ya CPC zimechapishwa hivi majuzi na Shirika la Uchapishaji wa Nyaraka Muhimu za Kamati Kuu ya CPC, zikiuzwa nchini kote China.

Juzuu hizo mbili zimekusanya hotuba na risala 136 alizotoa Xi Jinping katika miktadha ya kimataifa toka Machi, 2013 hadi Novemba, 2021.

Tokea Mkutano Mkuu wa 18 wa CPC, kamati kuu ya CPC ambayo Xi Jinping akiwa katibu mkuu wake inakabiliana na hali ya kimataifa yenye utatanishi na taabu kubwa, na changamoto na hatari kutoka nje ambazo hazikutokea hapo kabla, ikipanga mipango ya jumla kuhusu mambo makuu ya ndani na ya nje. Xi akiwa msanifu mkuu wa mambo ya kidiplomasia yenye umaalumu wa China, alifanya shughuli nyingi za kidiplomasia, na kukutana na viongozi wa nchi mbalimbali kwa mara nyingi, na kutoa hotuba na risala kwenye miktadha mbalimbali ya kimataifa, ambapo alitoa mawazo mapya na mapendekezo mapya mfululizo yanayoonesha umaalumu wa China na misingi ya zama tulizo nazo, na kuongeza uelewano na uungaji mkono wa jumuiya ya kimataifa kwa maendeleo ya China. Mawazo na mapendekezo hayo mapya yana maana muhimu kwa kuendeleza uhusiano wa kiwenzi wa dunia, kuhimiza ujenzi wa uhusiano wa aina mpya wa kimataifa, kuhimiza ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja, na kutukuza thamani ya pamoja ya binadamu juu ya amani, maendeleo, usawa, haki, demokrasia na uhuru.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha