Mjumbe wa China aonya juu ya vikwazo zaidi dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea (DPRK)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 12, 2022

UMOJA WA MATAIFA - Mjumbe wa Kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa, Zhang Jun Jumatano wiki hii ameonya dhidi ya majaribio ya kuiwekea vikwazo zaidi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea (DPRK).

“Mazungumzo na mashauriano ndiyo njia pekee sahihi ya kutatua suala la Peninsula ya Korea. Marekani inahusika moja kwa moja na suala hilo na inashikilia ufunguo wa kuvunja mkwamo huo. Kwa hivyo, inapaswa kuchukua hatua madhubuti kujibu kwa njia chanya wasiwasi wa DPRK na kuweka mazingira ya kuanza mapema mazungumzo” amesema Zhang.

Zhang ameliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwamba, ingawa upande wa Marekani unadai kuwa uko tayari kushiriki katika mazungumzo bila masharti, linapokuja suala la vitendo, unaendelea kuimarisha vikwazo na kutoa shinikizo. Hili ni wazi halijengi. "Rasimu ya azimio jipya lililopendekezwa na Marekani, na kuibua Sura ya VII ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa, inajikita zaidi katika kuendeleza vikwazo, ambayo si njia mwafaka ya kushughulikia hali ya sasa ya peninsula." Amesema.

Ameeleza kwamba, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa miaka mingi limepitisha maazimio mengi kuhusu suala hilo, ambayo licha ya kuidhinisha vikwazo, yamesisitiza pia haja ya kupatikana suluhu ya amani, kisiasa na kidiplomasia katika suala la nyuklia kwenye Peninsula ya Korea. Haya yote yanastahili kuzingatiwa sawa.

“Rasimu ya azimio lililowasilishwa na China na Russia ni kwa ajili hiyohiyo. Cha kusikitisha ni kwamba Marekani, ambayo ni mshika dau wa suala la kutoeneza silaha za DPRK, imefumbia macho mapendekezo yenye busara ya China na wajumbe wengine wa baraza husika, na inaendelea kupendeza ushirikina na nguvu ya uchawi ya vikwazo” anasema Zhang.

"Tunaamini kwamba ikiwa Marekani itabadili mtazamo wake hasi, inawezekana kwa wajumbe wa baraza hilo kufikia muafaka. Tunatumai wajumbe wa baraza hilo watazingatia kwa kina rasimu ya azimio la pamoja la China na Russia," anasema.

Suala la Peninsula ya Korea linapaswa kuangaliwa kihistoria na kwa kina ili kufahamu sababu na matokeo ya jambo hilo. Baada ya Mwaka 2018, kumekuwa na hali ya kupungua kwa misuguano. DPRK ilichukua mfululizo wa hatua za kukomesha nyuklia na kupunguza hali hiyo. Viongozi wa DPRK na Marekani walikutana nchini Singapore na kufikia makubaliano ya kuanzisha aina mpya ya uhusiano kati ya DPRK na Marekani, kujenga utaratibu wa amani kwenye peninsula, na kuendeleza mchakato wa kuondoa silaha za nyuklia. Katika hali ya kusikitisha, upande wa Marekani baadaye ulikengeuka msimamo wake, na haukujibu mipango chanya ya DPRK.

China ikiwa ni jirani wa karibu, ina wasiwasi mkubwa kuhusu hali ya Peninsula ya Korea, na daima imekuwa ikisisitiza kudumisha amani na utulivu kwenye peninsula hiyo, kuondoa silaha za nyuklia kwenye peninsula hiyo, na kutatua matatizo kwa njia ya mazungumzo na mashauriano.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha