Waziri Mkuu wa Misri awasili nchini Tunisia kuhudhuria mkutano wa kamati ya pamoja ya ushirikiano

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 13, 2022

Waziri Mkuu wa Tunisia Najla Bouden Romdhane (kulia) akikutana na Waziri Mkuu wa Misri Mostafa Madbouly kwenye uwanja wa ndege mjini Tunis, Tunisia, Mei 12, 2022. Mostafa Madbouly siku ya Alhamisi wiki hii amewasili Tunisia kuhudhuria mkutano wa kamati ya pamoja kuhusu kuimarisha ushirikiano baina ya nchi hizo mbili. (Ofisi ya Waziri Mkuu wa Tunisia/Kutumwa kwa Xinhua)

TUNIS - Waziri Mkuu wa Misri Mostafa Madbouly jana Alhamisi amewasili Tunisia kuhudhuria mkutano wa kamati ya pamoja kuhusu kuimarisha ushirikiano baina ya nchi hizo mbili.

Ofisi ya Rais wa Tunisia imesema katika taarifa yake kwamba Madbouly, anayeongoza ujumbe wa ngazi ya juu wa nchi yake, alipokelewa katika uwanja wa ndege na mwenzake wa Tunisia Najla Bouden Romdhane.

Katika ziara yake hiyo ya siku mbili, Madbouly amepanga kufanya mazungumzo na Rais wa Tunisia Kais Saied, Romdhane na maafisa wengine wakuu wa Tunisia.

Atahudhuria kikao cha 17 cha Kamati ya Juu ya Pamoja ya Misri na Tunisia kuhusu ushirikiano wa pande mbili.

"Kikao hiki kitakuwa fursa ya kuimarisha uhusiano wa kindugu na ushirikiano unaozifungamanisha nchi zetu mbili na kuziendeleza ili zifikie ngazi ya ushirikiano wa kudumu," Ofisi ya Rais wa Tunisia imesema.

Waziri Mkuu wa Tunisia Najla Bouden Romdhane (Mbele, kulia) akimkaribisha Waziri Mkuu wa Misri Mostafa Madbouly (Mbele, kushoto) kwenye uwanja wa ndege wa Tunis, Tunisia, Mei 12, 2022. (Ofisi ya Waziri Mkuu wa Tunisia/Kitini kupitia Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha