Kikosi cha Madaktari wa China chatoa dawa na vifaa vya tiba vya kujikinga na virusi vya korona kwa hospitali ya Tanzania

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 13, 2022

Kikosi cha 26 cha madaktari wa China nchini Tanzania kilitoa dawa na vifaa vya tiba vya kujikinga na virusi vya korona kwa hospitali ya taifa ya Muhimbili ya Tanzania vikiwemo vifaa vya kupumulia , mashine ya kutengeneza oksijeni na taa ya kuua vijidudu kwa mwanga wa UV.

Mkuu wa hospitali ya taifa ya Muhimbili ya Tanzania Lawrence Musero alishukuru sana upande wa China kwa kutoa msaada wa dawa na vifaa vya matibabu, na kusema kuwa kikosi cha madaktari wa China kimetoa mchango mkubwa kwa afya ya wananchi wa Tanzania, na msaada huo utaonesha umuhimu wake kwa ajili ya kuinua kiwango cha hospitali hii katika huduma ya matibabu na uwezo wa kupambana na virusi vya korona.

Kiongozi wa Kikosi cha 26 cha madaktari wa China nchini Tanzania Meng Yong alisema kuwa kikosi hicho kiliungwa mkono kwa nguvu kubwa na hospitali ya taifa ya Muhimbili ya Tanzania wakati wa kufanya kazi, alitumai dawa na vifaa vya matibabu hizi zinaweza kusaida hospitali hiyo kutatua matatizo katika kazi za ukingaji na udhibiti wa virusi vya korona na za kila siku. Katika siku za baadaye, kikosi kitaimarisha mawasiliano na Idara ya afya ya Tanzania, kutoa huduma nzuri kwa wenyeji na kufuata moyo wa kikosi cha madaktari wa China wanaotoa huduma za matibabu katika nchi za nje.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha