

Lugha Nyingine
Ofisi ya Afrika ya WHO yasema, Maambukizi ya virusi vya korona yaibuka tena kwenye eneo la Kusini mwa Afrika
Ofisa wa ofisi ya Afrika ya Shirika la Afya Duniani (WHO) anayeshughulikia kazi ya kukabiliana na hali ya dharura tarehe 12 kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwa njia ya video huko Brazzaville, mji mkuu wa Kongo-Brazzaville alisema, kutokana na athari ya virusi vya korona aina mpya ya Omicron na kulegezwa kwa hatua za kukinga na kudhibiti katika nchi nyingi, hivi karibuni maambukizi ya virusi vya korona yaliibuka tena kwenye eneo la Kusini mwa Afrika. Nchi zote zinatakiwa kuchukuatahadhari ili kukabiliana na wimbo jipya la maambukizi linalowezekana kutokea.
Taarifa iliyotolewa na ofisi ya Afrika ya WHO siku hiyo ilisema, katika wiki moja kabla ya tarehe 8, Mei, watu takriban 46,000 walithibitishwa kuambukizwa virusi vya korona, na idadi hiyo imeongezeka kwa asilimia 32 ikilinganishwa na ile ya wiki iliyopita. Kutokana na athari ya virusi vya korona aina mpya ya Omicron, ongezeko la kila wiki la idadi ya watu walioambukizwa nchini Afrika Kusini limeongezeka kwa mara tatu katika wiki tatu zilizopita. Na ongezeko la kila wiki la idadi ya watu wanaoambukizwa virusi pia limepanda juu katika Namibia na Swaziland.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma