Watu milioni 55 barani Afrika walikumbwa na hali ya umaskini kabisa kutokana na athari ya maambukizi ya virusi vya korona Mwaka 2020

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 16, 2022

Kamati ya Uchumi wa Afrika ya Umoja wa Mataifa ilitoa ripoti Tarehe 14 huko Dakar, mji mkuu wa Senegal ikisema kuwa kutokana na athari ya maambukizi ya virusi vya korona, watu milioni 55 hivi barani Afrika walikumbwa na hali ya umaskini kabisa Mwaka 2020.   

Mkutano wa 54 wa Mawaziri wa fedha, mpango na maendeleo ya uchumi wa Kamati ya Uchumi wa Afrika ya Umoja wa Mataifa ulifanyika kuanzia Tarehe 11 hadi 17 huko Dakar. Kamati hiyo ilitolea “ripoti ya uchumi ya Afrika ya Mwaka 2021” yenye mada ya “kukabiliana na changamoto za umaskini na udhaifu katika kipindi cha maambukizi ya virusi vya korona”, ambayo ilichambua sababu na matokeo ya hali mbaya ya umaskini barani Afrika wakati wa kutokea kwa maambukizi ya virusi vya korona.

Ripoti ilisema kuwa Mwaka 2020, takriban watu milioni 55 barani Afrika walikumbwa na hali mbaya zaidi ya umaskini kutokana na maambukizi ya virusi vya korona, ambayo iliathiri vibaya kazi ya kupunguza umaskini barani Afrika kwa zaidi ya miaka 20. Katika nchi za Afrika, watu wenye mali chache, mishahara midogo, mikopo yenye ukomo na ajira isiyo rasmi ni rahisi kukumbwa na hali mbaya ya umaskini baada ya kuathiriwa na maambukizi ya virusi vya korona.  

Ripoti hiyo ilisema kuwa mabadiliko ya hali ya hewa pia yameufanya umaskini uzidi kuwa mbaya na kuleta hali ya udhaifu wa kiuchumi, na nchi nyingi za Afrika zinakabiliwa na hali ya kujizama katika “kubeba madeni ya kupita kiasi”.  

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha