Mwaka wa Kwanza wa Chombo cha Tianwen-1 wa kutekeleza jukumu kwenye sayari ya Mars

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 16, 2022

Picha iliyochapishwa na CNSA tarehe 11, Juni, mwaka 2021 ikionesha chombo cha kwanza cha utafiti wa sayari ya Mars cha China pamoja na jukwaa la kutua kwake. (Picha inatoka CNSA ikichapishwa kwa kupitia Shirika la Habari la China Xinhua.)

Mwaka mzima umepita tangu chombo cha utafiti cha Tianwen-1 cha China kilipofika sayari ya Mars na kuanza kutekeleza jukumu lake. Jukumu hilo siyo tu ni alama ya hatua muhimu ya utafiti wa China kuhusu sayari wa Mars, bali pia limepata mafanikio mengi katika mwaka huo.

Tarehe 15, Mei, 2021, chombo cha utafiti cha Tianwen-1 kilitua kwenye tambarare ya Utopia, ambayo ni tambarare pana ya sayari ya Mars iliyochaguliwa kwa kutua kwake. Hii ni mara ya kwanza ya China kuwasilisha chombo cha utafiti kwenye sayari hiyo.

Mei 22, 2021 baada ya wiki moja, kigari cha utafiti wa sayari ya Mars Zhurong kilifika kwenye ardhi ya Mars kutoka jukwaa la kutua kwake. Tarehe 11, Juni, Mamlaka ya Anga ya Juu ya Kitaifa ya China ilichapisha picha ya kwanza iliyopigwa na Zhurong, ikiwa alama ya mafanikio makubwa ya kazi ya utafiti wa kwanza wa China kwenye sayari ya Mars.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha