Zaidi ya madereva 18,000 wa Tanzania wakamatwa kwa makosa ya barabarani kufuatia msako mkali

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 16, 2022

DAR ES SALAAM – Polisi wa Usalama Barabarani nchini Tanzania wamesema jana Jumapili kuwa madereva wapatao 18,410 walikamatwa katika muda wa chini ya miezi miwili kwa kuendesha magari kwa kasi na ulevi katika maeneo tofauti ya nchi hiyo ya Afrika Mashariki.

Kamanda wa Polisi wa Usalama Barabarani wa Tanzania Wilbroad Mutafungwa amesema madereva hao walikamatwa kwa kufanya makosa hayo ya barabarani katika msako mkali uliofanyika nchi nzima kati ya Aprili 1 na Mei 10.

"Kuendesha kwa mwendo kasi na ulevi ni vyanzo viwili vikubwa vya ajali za barabarani ambazo zinaripotiwa karibu kila siku barabarani," Mutafungwa amewaambia waandishi wa habari mkoani Geita, Kaskazini Magharibi mwa Tanzania.

Amesema madereva 17,916 walikamatwa kwa makosa ya mwendo kasi na madereva 494 walikamatwa kwa kuendesha magari wakiwa wamelewa.

Mutafungwa amesema, katika msako huo, magari 128,014 yalikaguliwa na askari wa usalama barabarani kati ya hayo magari 48,889 yalibainika kuwa na ubovu.

Amesema waendesha pikipiki takriban 38,276 nchi nzima pia walikutwa wakikiuka sheria za barabarani wakati wa msako huo, ikiwa ni pamoja na kupakia abiria zaidi ya mmoja na kutovaa helmeti za kujikinga.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha