

Lugha Nyingine
Namibia kuharibu zaidi ya dozi 300,000 za chanjo dhidi ya UVIKO-19 zilizokwisha muda wake kutokana kusuasua kwa watu kuchanja
WINDHOEK - Mkurugenzi Mtendaji wa Wizara ya Afya na Huduma za Kijamii ya Namibia Ben Nang'ombe amesema Jumatatu wiki hii kwamba nchi hiyo itaharibu zaidi ya dozi 300,000 za chanjo dhidi ya UVIKO-19 zenye thamani ya dola milioni 1.6 za Marekani ambazo muda wake wa matumizi umeisha.
Kwa mujibu wa Nangombe, dozi nyingine 42,000 za chanjo ya Astrazeneca pia muda wake wa matumizi utaisha ndani ya wiki chache zijazo.
Kwa mujibu wa Wizara ya Afya, hadi kufikia sasa nchi hiyo imechanja chanjo kikamilifu takriban watu 412,543, sawa na asilimia 23 ya jumla ya watu wote lengwa wanaokadiriwa kufikia milioni 1.78.
Nchi hiyo kwa sasa inakumbwa na ongezeko la idadi ya visa vipya vilivyothibitishwa vya UVIKO-19, vinavyosababishwa na virusi vya Korona aina ya Omicron BA.2 na BA.4 ambavyo vimegunduliwa nchini humo, huku Wizara ya Afya pia ikishuku kuwa Omicron BA.5 pia tayari inaambukizwa nchini Namibia.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma