

Lugha Nyingine
Mlemavu wa macho wa Rwanda afaulu kushinda taabu
![]() |
Rosette Uwifashije (wa kati) akiongoza wanafunzi kwenye kituo chake cha utoaji mafunzo kwenye Muhanga, Rwanda, Mei 14, 2022. (Picha/Xinhua) |
Rosette Uwifashije, mwanamke mwenye umri wa miaka 30 wa Rwanda alibadilika kuwa mlemavu wa macho kwa sababu ya ugonjwa mwaka 2000, lakini anawashangaza watu kuwa, anajua kutunga uzi kwenye tundu la sindano kwa haraka zaidi kuliko watu wanaoona .
Bibi Rosette ni mkazi wa eneo la Muhanga la Kusini mwa Rwanda, alifungua duka la ushonaji, akishona nguo za ya mitindo mbalimbali. Ingawa ana ulemavu, anatoa mafunzo kwa watu wengine pia.
Alipohojiwa na mwandishi wa habari wa shirika la habari la China Xinhua, Rosette alisema, alikuwa anajitahidi kujimudu maisha siku zote, na katika familia yake na kwenye jamii, alipaswa kukabiliana na aibu na kudhalilishwa .
Lakini baada ya rafiki yake kumsaidia kupata kazi kwenye Kituo cha Raslimali cha Masaka cha Kigali, mji mkuu wa Rwanda, maisha yake yamebadilika. Rosette ni mmoja wa wanawake walemavu wanaochaguliwa na kuungwa mkono na Umoja wa Walemavu wa Macho wa Rwanda (RUB) ili kujenga maisha yao ya kujitengemea na kuonesha uwezo wao kwa kupitia mradi huu wa ndoto ulioanzishwa na wafadhili.
Kituo hicho kinawasaidia kuponesha, kuwasaidia watu wenye matatizo ya kuona kujifunza kusoma na kuandika hati nundu , ili kubadilisha maisha yao. Kituo hicho pia kinawafundisha ufundi mpya wa kufanya kazi za kilimo na ufugaji, ili kuwasaidia kujenga uwezo wa kujitegemea.
Kutokana na msaada wa kituo hicho wa kutoa mafunzo ya kulengwa na kivitendo, Rosette alifaulu kushinda hali ya kujihurumia , na alianza kutembeatembea, na kushughulikia kazi ya kilimo na shughuli nyingine kwa kujitegemea.
Ili kushida taabu na kutimiza ndoto yake, baadaye Rosette alisoma somo la ushonaji kwa mwaka mzima kwenye shule ya ufundi wa kazi iliyoko eneo la Rubavu la Magharibi mwa Rwanda, akahitimu na kupata cheti.
Alisema, “Nina uwezo wa kushona nguo za mitindo tofauti kutokana na chaguo la kila mteja ,” aliongeza kuwa, ili kuongeza kipato chake, anawafundisha wengine kushona nguo. “Nimepata ufundi wa kutumia cherehani, ufundi huo kwa kawaida unawafaa watu wanaoona .”
Wanafunzi wake ni pamoja na walemavu wa macho waliopendekezwa na Umoja wa Malemavu ya Macho wa Rwanda.
Mnamo mwaka 2019, Rosette alipewa Tuzo ya Mawasiliano ya Vijana ya Rwanda kutokana na juhudi zake za kushinda changamoto za kuanzisha shughuli , pamoja na tuzo hiyo alipata motisha ya faranga za Kinyarwanda 500,000 (takriban Dola za Marekani 488), motisha hiyo ilihimiza maendeleo ya shughuli zake na mambo yake ya utoaji huduma.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma