

Lugha Nyingine
Kusoma Lugha ya Kichina kumewaletea wanafunzi wa Ghana nafasi nyingi za ajira
Kadiri ushirikiano wa kiuchumi unavyoendelea siku hadi siku kati ya China na Ghana, ndivyo wanafunzi wa Ghana wanaoanza kusoma Lugha ya Kichina wanaongezeka zaidi ili kujiandaa kwa ajili ya siku zao za baadaye.
Kwa muda mwingi, wanafunzi wa Ghana katika Chuo cha Confucius katika Chuo Kikuu cha Cape Coast, magharibi mwa Ghana, walijikita katika kusoma masomo ya Lugha ya Kichina na utamaduni wa jadi wa China, kutoka michezo ya Sanaa ya ngoma ya simba hadi ngonjera ya Kichina darasani.
Charles Delali Adegah ni mwenyeji mwenye umri wa miaka 30 aliyewahi kusoma masomo ya Lugha ya Kichina na utamaduni wa China na amepata shahada ya uzamili na kuwa mwalimu katika Chuo cha Confucius. Aliwaambia mwandishi wa Shirika la Habari la China, Xinhua kuwa aliposoma Lugha ya Kichina amepata furaha na kuona mustakabali wake.
"Kwa sababu nilisoma Lugha ya Kichina, nilipata nafasi ya kusoma bure nchini China. Nilipomaliza shahada yangu ya kwanza, niliishi nje ya nchi kwa mwaka mmoja, na niliajiriwa kuwa mkarimani na makampuni mbalimbali baada ya kurudi nchi yangu. Hivi sasa, baada ya kumaliza masomo ya shahada ya uzamili, nilipata mwaliko wa kuwa mwalimu katika Chuo cha Confucius katika Chuo Kikuu cha Cape Coast,” alisema.
Mwalimu huyo wa Chuo cha Confucius alieleza hali yake ngumu wakati aliposoma katika shule za msingi na sekondari kwa sababu ya matatizo ya kiuchumi, na aliwataka wanafunzi wa Ghana katika vyuo vikuu watumie fursa ya kusoma Lugha ya Kichina kutokana na mustakabali wake.
“Sisi sote tunajua kuwa makampuni mengi ya Ghana yanaongozwa na Wachina, na watu waliosoma Lugha ya Kichina ni rahisi kuajiriwa na makampuni hayo. Kwa hiyo, nataka kusema, ukipata nafasi ya kusoma Lugha ya Kichina, lazima uchukue nafasi hiyo, na ujifunze kwa bidii” Adfdvfdegah aliongeza.
“Nilipoanza kusoma lugha hiyo nilikutana na taabu kubwa, lakini kutokana na maendeleo katika masomo yangu, nilielewa kuwa kuna makampuni mengi hapa Ghana ambayo yangependa kuajiri Waghana wanaojua kuongea kwa Kichina. Sasa nina matarajio ya kwenda China kutalii na kuendelea na masomo yangu huko," alisema Belinda Koomson, mwanafunzi mwenye umri wa miaka ishirini hivi wa Chuo Kikuu cha Cape Coast, ambaye pia alikuwa amesoma masomo ya Lugha ya Kichina na utamaduni wa China katika miaka mitatu iliyopita, na kufikia daraja la kati.
Belinda alisema, Wachina wamekuja kujifunza lugha yetu, hivyo ni bora tujifunze lugha yao ili kuwasiliana nao na kufanya kazi pamoja kwa masikilizano .
Mkuu wa upande wa China wa Chuo hicho Ou Yamei alifahamisha kuwa, chuo hicho kimeweka masomo mbalimbali kama vile michezo ya jadi ya Wushu, sanaa ya mikono, maandiko ya Kichina, nyimbo na ngoma.
Ou alisema, chuo hicho kilichoanzishwa Mwezi Februari Mwaka 2016, kimeshuhudia wenyeji wengi waliobadilisha maisha yao kuwa mazuri baada ya kusoma Lugha ya Kichina.
Ou aliongeza kuwa, tutafanya juhudi za kuboresha kazi yetu ya mafunzo na kuweka masomo ya hali ya juu kwa wanafunzi wetu ili kukidhi mahitaji yao yanayoongezeka siku hadi siku.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma