Kituo cha Kibiashara cha Kimataifa kilichowekezwa na China chatarajiwa kuongeza hadhi ya Kenya kuwa kitovu cha kikanda

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 19, 2022

NAIROBI - Kituo cha Kibiashara cha Kimataifa kilichowekezwa na China mjini Nairobi, Mji Mkuu wa Kenya, ambacho kinatarajiwa kufunguliwa Mwezi Septemba mwaka huu, kitakuza hadhi ya Kenya kuwa kitovu cha kibiashara cha kikanda.

Shamim Malowa, msimamizi wa masoko wa Kampuni ya Kimataifa ya Biashara zisizohamishika ya AVIC-Kenya, amewaambia waandishi wa habari jijini Nairobi kwamba nakshi za mwisho kwa sasa zinaendelea kuwekwa kwenye nyumba za makazi kwenye jengo la ghorofa 31, jengo moja la ofisi lenye ghorofa 42 na duka kubwa la reja reja.

"Tunaleta huduma za kiwango cha kimataifa, ikimaanisha kuwa tumeshirikiana na chapa maarufu duniani katika eneo moja," Malowa amesema wakati wa kongamano la kikanda kuhusu mali zisizohamishika.

Amebainisha kwamba hoteli ya nyota tano ya J.W Marriot yenye ghorofa 35 itafunguliwa na kuanza kutoa huduma katika robo ya mwisho ya Mwaka 2023.

Jengo hilo kubwa linaloitwa AVIC Towers, linajengwa na kampuni kutoka China ya Aviation Industry Corporation of China (AVIC)

Malowa amebainisha kuwa maghorofa ya GTC yatatumika kwa hoteli, ofisi, maegesho, maduka makubwa, mikuktano na makazi (HOPSCA).

"Kwa hivyo tunawapa Wakenya na kila mtu anayekuja nchini kufanya biashara, aina hiyo ya uzoefu ambayo ni ya kiwango cha kimataifa na yenye ufanisi," Malowa amesema.

Ameweka wazi kuwa mradi huo unatarajiwa kuvutia makampuni ya kimataifa kuhamia Nairobi kutokana na viwango vyake vya kisasa vya ujenzi.

Kwa mujibu wa afisa huyo wa AVIC, eneo la jengo la GTC karibu na Barabara Kuu ya Nairobi iliyojengwa kwa uwekezaji wa Wachina sasa linakuwa eneo linalofaa kwa watalii wa biashara na burudani.

"Tupo katikati ya maeneo tofauti ya kufikika kwa urahisi na hivyo tutavutia watu wanaotafuta ufanisi kwa wakati, pamoja na tija kwa watu wanaoishi na kufanya kazi kwenye majengo hayo," Malowa amesema na kubainisha kuwa mradi wa GTC utainua wasifu wa Nairobi kwa kubadilisha mandhari na kuifanya kuwa kitovu cha uwekezaji na utalii.

Malowa amesema kuwa mradi wa GTC tayari umehamasisha miji mingine ya Afrika kujenga mradi kama huo.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha