

Lugha Nyingine
Rais wa Zimbabwe atetea uwekezaji wa China barani Afrika dhidi ya uchochezi wa nchi za Magharibi
HARARE - Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa amepongeza uwekezaji wa China kwa kubadilisha hali ya uchumi katika nchi yake na maeneo mbalimbali ya Afrika, huku akizikosoa nchi za Magharibi kwa kupora rasilimali za Afrika kwa miongo kadhaa.
Katika safu yake ya makala ya kila wiki kwenye gazeti linaloendeshwa na serikali la The Sunday Mail, Mnangagwa amesema kuwa kuchelewa kwa uwekezaji wa China kuingia barani Afrika kumefanya mabadiliko makubwa kwa muda mfupi.
"Wameleta thamani na ajira kwa uchumi na jamii zetu, kuwezeshwa kupita ushirikiano wa kiwenzi wenye maumivu makali ambao haujawahi kutokea katika historia yetu yenye matatizo katika bara letu," ameandika.
"Tumeona mitaji ya China ikisaidia miradi ya kihistoria katika Bara la Afrika," amebainisha na kuongeza, "Hapa Zimbabwe, China imesaidia kufadhili na kutekeleza miradi kadhaa katika sekta ya nishati, usafiri wa anga, maji, mali isiyohamishika, kuongeza thamani ya viwanda, madini na ulinzi."
"Haya yote yamelinda na kuimarisha uhuru wetu huku yakibadilisha muundo wa uchumi wetu katika msimu huu wa vikwazo vya kuadhibu kutoka nchi za Magharibi," amesema.
Mnangagwa amesema, hata hivyo, nchi za Magharibi, hazijafurahishwa na alama ya China katika bara hilo na kuwashauri viongozi wa Afrika kuwa makini na Wachina, pamoja na Warusi, Wahindi, Wabrazil na Waarabu.
"Ikiwa ni pamoja na hapa Zimbabwe, tumeona baadhi ya serikali za Magharibi zikifadhili vikundi kadhaa vya uongo vya utetezi wa mazingira na uchimbaji madini ambavyo vinataka kuchochea jamii dhidi ya maslahi ya uchimbaji madini yasiyo ya Magharibi," amesema. "Ushauri wao kwetu ni wa uwongo na wa kejeli; tunaukataa kwa dharau kabisa inayoustahili."
Akitoa mfano wa Mgodi wa Bikita, uliopo katika milima ya Bikita katika Jimbo la Masvingo nchini Zimbabwe, amesema nchi za Magharibi ndizo zinazofadhili upinzani ili kupinga uwepo wa wachimbaji kutoka China huko Bikita kwa vile madai ya jamii wenyeji ni ya kizamani na yaliyoanza wakati migodi hiyo ikiendeshwa na wamiliki wa Magharibi.
"Kwa kushangaza, Mgodi wa Bikita ulichukuliwa na mwekezaji wa China mapema katika mwaka, baada ya kumilikiwa na kunyonywa na maslahi ya Magharibi kwa miaka mingi tangu rasilimali hiyo ilipogunduliwa huko nyuma enzi za ukoloni."
"Wakati mali hizo za uchimbaji madini zikiwa mikononi mwa nchi za Magharibi, muda mrefu kabla ya uhuru wetu na baada ya hapo, hata mara moja jamii za wenyeji hazikufaidika. Wala jamii za wenyeji hazikuchochewa, kuhamasishwa na kufadhiliwa kulinda rasilimali na mazingira yao duni," amesema.
Amesema, mgodi huo ulikuwa ukingoni kuanguka hadi pale mwekezaji mpya alipouokoa na kupanua shughuli zake kwa mtaji mpya, hivyo kutengeneza fursa za ajira kwa Wazimbabwe.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma