Idadi ya waliouawa kwa kupigwa risasi katika shule ya Msingi huko Texas, Marekani yafikia 21, wakiwemo watoto 18

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 25, 2022

HOUSTON - Idadi ya vifo vinavyotokana na kupigwa risasi kwenye shule ya msingi katika Jimbo la Texas nchini Marekani imeongezeka hadi kufikia 21, wakiwemo watoto 18, Seneta wa jimbo hilo amesema jana Jumanne, akinukuu taarifa ya Idara ya Usalama wa Umma ya Texas.

Mapema siku hiyo, Gavana Greg Abbott alisema katika mkutano na waandishi wa habari kwamba, mtu mwenye bunduki Jumanne mchana aliingia katika shule ya msingi huko Uvalde katika Jimbo la Texas nchini Marekani na kuwaua watoto 14 na mwalimu mmoja.

Mshambuliaji huyo alikuwa kijana mwenye umri wa miaka 18, ambaye aliacha gari lake na kuingia shuleni akiwa na bunduki aina ya pistol na pengine rifle, Abbott amesema, akiongeza kuwa "alipiga risasi na kuwaua wanafunzi 14 na mwalimu kwa njia ya kutisha, isiyoeleweka."

Polisi wanaaminiwa kumuua mshambuliaji huyo.

“Watoto wawili waliopigwa risasi walikuwa tayari wamefariki wakati waokoaji walipowasili katika Hospitali ya Uvalde Memorial” Adam Apolinar, afisa mkuu wa uendeshaji wa hospitali hiyo, alinukuliwa na Gazeti la The New York Times akisema mapema mchana.

Hospitali ya Chuo Kikuu cha San Antonio ilipokea majeruhi wawili kutokana na kupigwa risasi, ikiandika kwenye mtandao wa Twitter kwamba wagonjwa hao, mtoto mmoja na mtu mzima mmoja, "kwa sasa wanapokea matibabu na uangalizi kwa hivyo hakuna mazingira ya kutoa taarifa zaidi kwa sasa."

Shirika la Shule Binafsi katika Wilaya ya Uvalde huko Texas limesema linasitisha shughuli zote za masomo baada ya tukio hilo kutokea katika Shule ya Msingi ya Robb. "Shughuli zote za wilaya na vyuo, programu za baada ya masomo, na hafla zimesitishwa," ujumbe kwenye mtandao Twitter umeeleza.

Idara ya Vilevi, Tumbaku, Silaha na Vilipuzi (ATF) inawasaidia polisi wa eneo hilo katika uchunguzi wa tukio hilo la ufyatuaji risasi. "Mawakala Maalum kutoka Kitengo chetu cha Operesheni cha Houston wanajitolea kusaidia Idara ya Polisi ya Uvalde (UPD) katika uchunguzi wao," Msemaji wa ATF Erik Longnecker amekiambia Kituo cha Televisheni cha CNN.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha