Meli iliyowabeba wahamiaji haramu yazama katika bahari ya eneo la Tunisia na kusababisha kifo cha mtu mmoja na wengine 75 wasiojulikana walipo

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 26, 2022

Msemaji wa Kikosi cha ulinzi wa umma cha Kitaifa cha Tunisia Bw.Jebable alisema tarehe 25 kuwa meli moja iliyowabeba wahamiaji haramu ilizama katika bahari ya eneo la Tunisia na kusababisha kifo cha mtu mmoja na wengine 75 wasiojulikana walipo.

Jebable alisema kwenye akaunti za mitandao ya kijamii kuwa meli hiyo iliyowabeba wahamiaji haramu wapatao 100, iliondoka kutoka bahari karibu na mji wa Zuwara, magharibi mwa Libya, na ilipojaribu kwenda Italia kwa kupitia bahari ya Mediterania ilizama katika bahari karibu na mji wa bandari wa Sfax, mashariki mwa Tunisia.

Jababli alisema kuwa watu 24 walionusurika waliokolewa, waokoaji wameokoa mwili wa mtu mmoja, na uokoaji kwa watu 75 wasiojulikana walipo bado unaendelea,

Katika miezi kadhaa ya hivi karibuni, idadi ya watu wanaojaribu kuingia kiharamu katika nchi ya Italia kutoka Tunisia na Libya imeongezeka na kumekuwa na makumi ya watu wakizama kwenye bahari ya eneo la Tunisia tokea Mwezi Aprili. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha