Serikali ya Ethiopia yapongeza juhudi za makampuni ya China za kuwajibika kijamii

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 26, 2022

Wawakilishi wakikata utepe wakati wa uzinduzi wa Barabara ya Mekanisa Abo mjini Addis Ababa, Ethiopia, Mei 25, 2022. Serikali ya Ethiopia Jumatano wiki hii imepongeza makampuni ya China kwa jitihada zao za kuwajibika kijamii katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki. Kauli hiyo imetolewa na Yasmin Wohabrebbi, Naibu Meya wa Addis Ababa, wakati wa uzinduzi wa Barabara ya Mekanisa Abo mjini. Mradi huo umefadhiliwa na kujengwa na Kampuni ya Uhandisi na Ujenzi ya China (CCECC), ikiwa ni sehemu ya jitihada zake za kuwajibika kijamii. (Xinhua/Wang Ping)

ADDIS ABABA - Serikali ya Ethiopia Jumatano wiki hii imepongeza kampuni za China kwa juhudi zao za kuwajibika kijamii katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki.

Kauli hiyo imetolewa na Yasmin Wohabrebbi, Naibu Meya wa Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia, wakati wa uzinduzi wa Barabara ya Mekanisa Abo mjini Addis Ababa. Mradi huo umefadhiliwa na kujengwa na Kampuni ya Uhandisi na Ujenzi ya China (CCECC), ikiwa ni sehemu ya jitihada zake za kuwajibika kijamii.

"Aina hii ya miradi ni sehemu ya wajibu wa kijamii wa makampuni ya kimataifa, kama vile CCECC, ni jambo ambalo serikali inahimiza sana kwa sababu maendeleo yote hayawezi kusimamiwa na serikali pekee," Wohabrebbi amesema.

Amesema serikali inahimiza ushiriki wa sekta binafsi na makampuni mengine ya kimataifa kufanya shughuli kama hizo kwani zitatimiza matarajio ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya nchi hiyo.

"Katika kipindi cha miaka mitatu au minne iliyopita, mengi yametokea nchini Ethiopia ambapo ushiriki wa makampuni ya kibiashara katika kuwajibika kijamii umeongezeka," amesema.

Amebainisha kuwa barabara hiyo mpya iliyojengwa na CCECC itakuwa na umuhimu mkubwa katika kuboresha maisha ya kila siku ya jamii ya eneo hilo.

Kwa mujibu wa takwimu kutoka kwa uongozi wa wilaya wa eneo hilo, Barabara mpya ya Mekanisa Abo iliyozinduliwa itahudumia takriban wakazi 30,000, na hatimaye kuboresha mtandao wa barabara na maisha yao.

Yang Yihang, Konsela wa Masuala ya Uchumi na Biashara wa Ubalozi wa China nchini Ethiopia, kwa upande wake amehimiza makampuni ya China yanayofanya kazi nchini Ethiopia kuimarisha zaidi wajibu wao wa kijamii na kuchangia katika kuboresha maisha ya watu nchini Ethiopia.

"CCECC pamoja na makampuni mengine mengi ya China yametekeleza kikamilifu wajibu wao wa kijamii na kutoa michango katika ujenzi wa miundombinu, kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wenyeji, kutengeneza fursa za ajira, na kuboresha maisha ya watu nchini Ethiopia," Yang amesema.

Guo Chongfeng, Meneja Mkuu wa CCECC tawi la Ethiopia, amesema kampuni hiyo inalenga kuboresha maisha ya jamii za Ethiopia ikiwa ni sehemu ya ushiriki wake katika nchi hiyo.

"Ethiopia ndipo tunapopaendeleza, ustawi wa Ethiopia ndiyo tunataka, na watu wa Ethiopia ndiyo tunaowajali. Wakati inaboresha hali ya miundombinu barani Afrika, CCECC daima inatimiza wajibu wa kijamii kwa Ethiopia," amesema.

Yasmin Wohabrebbi, Naibu Meya wa Addis Ababa, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Barabara ya Mekanisa Abo mjini Addis Ababa, Ethiopia, Mei 25, 2022. (Xinhua/Wang Ping)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha