Mashindano ya “Daraja la Lugha ya Kichina” yakuza urafiki kati ya China na Misri

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 27, 2022

Aya Ibrahim, msichana wa Misri ambaye alishinda tuzo ya juu katika Mashindano ya “Daraja la Lugha ya Kichina” yalilomalizika hivi karibuni, akizungumza na mwandishi wa habari wa Xinhua huko Cairo, Misri, Mei 24, 2022.(Xinhua/Sui Xiankai)

Jumanne wiki hii, msichana huyo pamoja na washindi wengine saba wa mashindano hayo, walikutana na Balozi wa China nchini Misri Liao Liqiang na kumwelezea hadithi zao za kusoma Lugha ya Kichina.

Ibrahim alisema mwanzoni aliona kuwa ni vigumu sana kusoma Lugha ya Kichina, lakini baadaye alishiriki katika shughuli mbalimbali kuhusu Lugha ya Kichina katika Chuo cha Confucius katika Chuo Kikuu cha Cairo, shughuli hizo zilizohusu sanaa ya China ya ukataji wa karatasi na kufuma nguo za China zilinifurahisha na kunisaidia kushinda taabu zote katika kusoma Lugha ya Kichiba.

Msichana huyo wa Misri alisisitiza tumaini lake la kuchangia kuzidisha urafiki kati ya China na Misri, na kupata nafasi ya kwenda China kumaliza masomo yake ya shahada ya uzamili.

Aya Magdy, mshindi mwingine aliyepata tuzo ya nafasi ya kwanza katika mashindano hayo, pia alisema kusoma Lugha ya Kichina kumebadilisha tabia yake na maisha yake.

Magdy anatarajia kuwa mwalimu wa lugha na kuwawezesha watu waijue zaidi China na utamaduni wake.

Balozi wa China alisema, ameguswa na hadithi zao na kuona fahari, akibainisha Mei 30 ni siku ya Maadhimisho ya miaka 66 ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya Misri na China.

Balozi huyo alisema, “ maendeleo ya uhusiano wa wenzi wa kimkakati kati ya China na Misri yanahitaji watu wa nchi hizi mbili kujishirikisha na kutoa mchango, hasa yanahitaji vijana wa nchi hizo mbili warithisha na kufanya uvumbuzi”.

Mashindano ya “Daraja la Lugha ya Kichina” yaliyofanyika katika Chuo Kikuu cha Ain Shams huko Cairo Mei 14, yaliwavutia washiriki wanafunzi 23 kutoka vyuo vikuu 18 vya Misri. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha