Tukio la kufyatua risasi kwenye tamasha la muziki la Oklahoma, Marekani lasababisha kifo cha mtu mmoja na wengine saba kujeruhiwa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 30, 2022

Vyombo vya Habari vya Marekani vilitoa habari kuwa tukio la kufyatua risasi lilitokea alfajiri ya tarehe 29 kwenye tamasha la muziki nje ya nyumba huko Oklahoma, Marekani, na lilisababisha kifo cha mtu mmoja na wengine saba kujeruhiwa, ikiwa ni pamoja na watoto wawili wasiofikia umri wa miaka 18.

Habari zilisema kuwa tukio hilo lilitokea katika Uwanja wa mji mkongwe wa Taft, mji mdogo karibu na Tulsa, ambao ni mji wa pili kwa ukubwa wake katika jimbo hilo, wakati watu 1,500 hivi walishiriki kwenye tamasha hilo la muziki. Tukio hilo lilidhaniwa kusababishwa na ugomvi.

Ofisi ya Uchunguzi ya Oklahoma ilisema bado hakuna mtuhumiwa anayekamatwa.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha