

Lugha Nyingine
Gazeti la New York Times: Marekani imevunjwa kwa kiwango cha kutoweza kurekebishwa kufuatia matukio ya watu wengi kuuawa kwa risasi
Mishumaa ikiwa imewashwa wakati wa mkesha wa kuomboleza waathirika wa shambulio la risasi kwenye halaiki katika shule huko Town Square, Uvalde, Texas, Marekani, Mei 29, 2022. Takriban watoto 19 na watu wazima wawili waliuawa kwa kupigwa risasi katika Shule ya Msingi ya Robb huko Uvalde Tarehe 24 Mei. (Xinhua/Wu Xiaoling)
NEW YORK – Gazeti la New York Times la Marekani mwishoni mwa wiki iliyopita liliandika kwamba, waathiriwa wa matukio ya mara kwa mara ya ufyatuaji risasi yanayongezeka ni uharibifu wa dhamana katika vita baridi vya wenyewe kwa wenyewe nchini Marekani, ingawa baadhi ya wanachama wa Chama cha Democrats wanakataa kukiri hivyo, achilia mbali kukabiliana na tatizo.
“Katika nchi hii, upatikanaji wa silaha ni, kwa haki, suala la umuhimu wa uhai. Bunduki ni mdhamini dhidi ya unyanyasaji wa serikali, na unyanyasaji wa serikali unajumuisha majaribio ya kudhibiti bunduki” inasomeka makala ya mwandishi Michelle Goldberg.
Kwa mujibu wa makala hayo, haitawezekana kufanya chochote kuhusu bunduki nchini Marekani, angalau katika ngazi ya taifa, ilimradi tu Chama cha Democrats kinategemea ushirikiano na Chama cha Republican, ambacho hakina nia ya kuruhusu Chama cha Democrats kupitisha hata hatua za kawaida kama vile ukaguzi wa historia ya mtu kabla ya kununua bunduki.
Mtu anaonekana pichani akiomboleza waathirika wa shambulizi la risasi kwenye halaiki katika shule huko Town Square, Uvalde, Texas, Marekani, Mei 28, 2022. (Xinhua/Wu Xiaoling)
"Jambo la kuogofya ni kwamba kadiri Marekani inavyozingirwa na ghasia zisizo na maana, ndivyo kundi la kutetea silaha la mrengo wa kulia nchini Marekani linavyoimarishwa. Mauzo ya bunduki huongezeka baada ya watu wengi kuuawa kwa kupigwa risasi," inasomeka makala hiyo.
"Bunduki sasa ndiyo chanzo kikuu cha vifo vya watoto wa Marekani. Wahafidhina wengi wanaona hii kama gharama inayostahili kulipwa kwa aina yao ya uhuru. Taasisi zetu zinawapa wahafidhina hawa uwezo usiyo na uwiano wa kuamua kama watashinda au kushindwa kwenye uchaguzi," inaeleza makala hiyo.
Kwa hivyo miongoni mwa waliberali, kuna hisia nyingi za kukata tamaa, inasomeka makala hiyo, huku ikibainisha kuwa, "Marekani ni mgonjwa sana, imevunjika sana. Labda haiwezi kurekebishwa."
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma