Rais Xi Jinping ahimiza juhudi za kujenga China nzuri

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 06, 2022

Picha iliyopigwa kutoka juu Septemba 26, 2021 ikionyesha mwonekano wa Nyumba za jani za Fuligong kwenye Bustani ya Mimea ya Kunming huko Kunming, Mkoa wa Yunnan nchini China. (Xinhua/Jiang Wenyao)

SHENYANG - Rais wa China Xi Jinping jana Jumapili alihimiza juhudi za kujenga China nzuri ambayo binadamu wanaishi katika hali ya kupatana na mazingira ya asili na kuchangia zaidi katika ujenzi wa pamoja wa dunia yenye usafi na inayopendeza.

Xi, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China, aliyasema hayo katika barua ya pongezi kwa Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira yaliyofanyika Shenyang, Mkoa wa Liaoning, Kaskazini Mashariki mwa China.

“Mazingira ya kiikolojia ndiyo msingi wa maisha na maendeleo ya binadamu, na kudumisha mazingira ya asili ni matarajio ya pamoja ya watu wa nchi zote”, Xi alisema.

China imetilia maanani maendeleo ya ujenzi wa mazingira ya kiikolojia na imefanya kazi ya msingi, ya uanzilishi na ya muda mrefu tangu Mkutano Mkuu wa 18 wa CPC ulipofanywa, Xi alisema huku akisisitiza kuwa mabadiliko ya kihistoria, kimageuzi na ya kina yamepatikana.

Katika safari mpya ya kujenga nchi yenye mambo ya kisasa ya kijamaa, China itadumisha azimio la kimkakati la kuwezesha maendeleo ya kiikolojia, kuhimiza maendeleo ya kiuchumi na kijamii yasiyoleta uchafuzi mwingi kwa mazingira, kufanya mpango wa jumla wa kudhibiti uchafuzi wa mazingira, ulinzi wa ikolojia na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Xi alitoa wito wa kuchukua hatua za pamoja na madhubuti kutoka kwa jamii nzima katika kulinda mazingira ya asili na kuacha nchi nzuri yenye anga ya buluu, ardhi yenye ustawi wa mimea na miti na maji safi kwa vizazi vijavyo.

Han Zheng, Mjumbe wa Kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC, alishiriki kwenye hafla ya ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku ya Mazingira na kutoa hotuba.

Han alihimiza juhudi za kuhimiza maendeleo ya kazi zote yasiyoleta uchafuzi mwingi kwa mazingira, na kufanya uratibu katika ulinzi wa mazingira na maendeleo ya uchumi.

Alisema China itafikia kilele na usawazishaji wa hewa ya kaboni kwa njia ya umakini na yenye utaratibu katika mchakato huo, kuhakikisha usalama wa nishati, usalama wa viwanda na minyororo ya ugavi, na usalama wa chakula, pamoja na kuhakikisha maisha ya kawaida ya watu.

China imekuwa ikiadhimisha Siku ya Mazingira kila mwaka tokea Mwaka 2017, ambayo mwaka huu imebeba kaulimbiu ya "Kushirikiana kwa pamoja Kujenga Dunia Safi na Nzuri." 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha